Main Title

source : ParsToday
Jumatatu

27 Januari 2020

07:50:33
1005833

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema Marekani ndiyo chimbuko la matatizo yote yanayoikabili Lebanon.

(ABNA24.com) Sheikh Naim Qassem amesema hayo katika radiamali yake kwa matamshi ya Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ambaye amedai kuwa Washington ina wasi wasi kuhusu nafasi ya Hizbullah katika serikali mpya ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Amesema, "matatizo na changamoto zote zinazoikabili Lebanon hivi sasa zinatokana na sera ghalati ya uingiliaji wa mambo ya ndani ya nchi ya Washington. Marekani haina haki ya kuzungumza chochote kuhusu muundo wa serikali ya nchi hii."

Sheikh Naim Qassem ameeleza bayana kuwa, harakati ya Hizbullah kwa kushirikina na makundi mengine ya kisiasa na taasisi za serikali nchini Lebanon zinafanya kazi bega kwa bega kwa maslahi ya wananchi na kwamba serikali ya Beirut haipaswi kushughulishwa na matamshi ya viongozi wa nchi za kibeberu.

Kwengineko katika hotuba yake, Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah amesema kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) pamoja na wafuasi wake nchini Iraq ni mwanzo wa kufikia tamatati uwepo wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi.

Ameongeza kuwa, njia ya muqawama itaendelezwa kwa nguvu zote katika eneo baada ya mauaji hayo ya kigaidi yaliyofanywa na jeshi la Marekani karibu na Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Baghdad nchini Iraq mnamo Januari 3. Aidha amepongeza jibu kali lilitolewa na Iran la kupiga kwa makombora kambi za jeshi za Marekani nchini Iraq, kulipiza kisasi cha damu ya Jenerali Soleimani na wenzake.

...........
340