Main Title

source : ParsToday
Jumatatu

27 Januari 2020

08:04:40
1005853

Hizbullah ya Iraq yasisitiza tena kuwa tayari kuwakabili askari vamizi wa Marekani

Kwa mara nyingine tena Harakati ya Muqawama ya Hizbullah nchini Iraq imetangaza azma yake ya kutoa pigo dhidi ya askari wa Kimarekani kwa kuanzisha vita vya kushtukiza dhidi ya askari hao ndani ya nchi hiyo ya Kiarabu na eneo zima la Asia Magharibi.

(ABNA24.com) Komanda wa operesheni maalumu wa harakati ya Hizbulla ya Iraq ametangaza kuwa, wanamuqawama wa harakati hiyo wanafuatilia kwa karibu harakati zote za askari hao vamizi wa Marekani kwa ajili ya kutoa pigo dhidi yao.

Hii ni katika hali ambayo kikosi cha makombora cha harakati hiyo pia kimetoa taarifa inayosisitiza kuwa kimejiweka tayari kwa ajili ya kutekeleza mashambulizi makali dhidi ya maadui na kuwageuza kuwa majivu.

Kikosi hicho cha makombora kimefafanua zaidi kwamba hakuna ngao yoyote ya makombora ikiwemo ya Patriot ya Marekani, inayoweza kuzuia mashambulizi ya harakati hiyo.

Kufuatia shambulizi la kigaidi lililofanywa na askari wa Marekani tarehe tatu ya mwezi huu mjini Baghdad na kupelekea kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC pamoja Abu Mahdi al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Iraq maarufu kwa jina la Hashdu sh-Sha'abi, wawakilishi wa bunge la Iraq walipitisha muswada wa kuwatimua askari vamizi wa Kimarekani kutoka ardhi ya nchi hiyo.

Viongozi wengi wa Iraq akiwemo Adil Abdul-Mahdi, Waziri Mkuu wa serikali ya sasa, sambamba na kuunga mkono muswada huo, wamekuwa wakisisitizia umuhimu wa kuondoka haraka nchini humo askari hao wa Kimarekani.

Katika uwanja huo Ijumaa iliyopita raia wa Iraq walishiriki katika maandamano ya mamilioni ya watu mjini Baghdad wakitaka kuondoka nchini humo askari hao vamizi.

............
340