Main Title

source : ParsToday
Jumatatu

27 Januari 2020

08:04:46
1005854

Wamarekani wafanya maandamano katika majimbo 40 kupinga siasa mbovu za Trump dhidi ya Iran

Raia wa Marekani katika majimbo 40 ya nchi hiyo wamemiminika mitaani katika maandamano makubwa ya kupinga siasa mbovu za serikali ya Rais Donald Trump dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

(ABNA24.com) Mtandao wa habari wa Times Union umeripoti kwamba raia wa Marekani pamoja na wanaharakati wanaopinga vita, wamefanya maandamano katika zaidi ya majimbo 40 ya nchi hiyo kupinga siasa za kupenda vita za Washington dhidi ya Iran.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo maandamano hayo pia yamefanyika katika viunga vya jimbo la New York, ambapo washiriki wake wamepinga vitisho vya Marekani dhidi ya Iran.

Aidha waandamanaji wa mji wa Potsdam, New York sambamba na kupiga nara ya 'Hakuna vita na Iran', wamelaani siasa za serikali ya nchi hiyo dhidi ya Tehran. Mmoja wa washiriki wa maandamano hayo amenukuliwa akisema: "Sisi Wamarekani tunapinga vita."

Hii ni katika hali ambayo baadhi ya waandamanaji walipiga kambi mbele ya ikulu ya Marekani (White House) kama ambavyo walimtaka Rais Donald Trump kuhitimisha mzozo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kuondoa askari wa nchi hiyo Iraq na maeneo mengine ya Asia Magharibi.

Aidha washiriki wengine wa maandamano hayo wameonyesha kuchukizwa sana na uongo uliosemwa na serikali ya Washington kuhusiana na hasara iliyolikumba jeshi la Marekani katika shambulio la makombora la Iran kwenye kambi ya jeshi ya Ain Al-Assad nchini Iraq.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imeendelea kutoa taarifa za majeraha ya idadi kubwa ya askari wa nchi hiyo. Katika uwanja huo tarehe 24 ya mwezi huu wizara hiyo ya Ulinzi ya Marekani ilikiri kwamba: "Hadi sasa askari wengine 34 wa Kimarekani walipatwa na matatizo ya ubongo katika shambulio la Iran dhidi ya kambi ya jeshi la Ain Al-Assad."

...........
340