Main Title

source : ParsToday
Jumapili

2 Februari 2020

07:54:28
1007081

Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria uwezo wa kujihami wa Iran na kusema: "Jeshi la nchi kavu la Iran ni la tano kwa uwezo wa nchi kavu duniani."

(ABNA24.com) Akizungumza wakati alipotembelea  Kituo 01 cha Mafunzo ya Kijeshi mjini Tehran, Brigedia Jenerali Kiumars Heidari ameongeza kuwa, majeshi ya nchi kavu ndiyo ambayo humaliza kila vita na kuongeza kuwa: "Uwezo wa mizinga wa Jeshi la Nchi Kavu la Iran ni moja ya misingi ya uwezo wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran."

Brigedia Jenerali Heidari aidha amesisitiza kuwa Uislamu ni dini ya ubinadamu na kuongeza kuwa, lengo la masomo katika Uislamu ni kupata saada na kuondokana na ujahili. Ameendelea kusema kuwa, mmoja kati ya watu ambao wamelelewa katika mafundisho matukufu ya Uislamu ni Luteni Jenerali Qassem Soleimani, kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeuawa shahidi mwezi Januari katika hujuma ya kigaidi ya Marekani nchini Iraq.

Kwingineko, Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Amir Hatami amesema taifa la Iran katu halitasalimu amri mbele ya mdola ya kibeberu. Aidha ametoa onya kwa maadui wa Iran na kusema: "Iwapo yeyote atajaribu kukiuka usalama wa watu wa Iran na itikadi zao, basi atapata jibu kali kutoka Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Hali kadhalika ameashiria kuwadia maadhimisho ya mwaka wa 41 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema: "Mshikamano na umoja wa watu wa Iran ni sababu kuu ya kufeli njama za madola ya ubeberu na uistikbari wa kimataifa."

...........
340