Main Title

source : ParsToday
Jumapili

2 Februari 2020

07:54:29
1007082

IRGC: 'Majeraha ya Ubongo' ni njia ya kuficha idadi ya askari wa Marekani waliouawa katika hujuma ya makombora ya Iran

Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema madai ya Marekani kuhusu idadi kubwa ya wanajeshi wake waliopata 'majeraha ya ubongo' kufuatia makombora ya Iran ya ulipizaji kisasi yaliyolenga kituo cha kijeshi cha Ain al Assad nchini Iraq ni njia ya kuficha idadi ya wanajeshi waliouawa katika oparesheni hiyo.

(ABNA24.com) Katika makala aliyoandika katika gazeti la Vatan-e-Emrooz la Iran toleo la Jumamosi, Msemaji wa IRGC Brigedia Ramezan Shariff amesema: "Tumefikia natija kuwa wakati Marekani inaposema wanajeshi wake wamepata 'majeraha ya ubongo' kufuatia hujuma dhidi ya kituo cha Ain al Assad, kauli hiyo inamaanisha wanajeshi wa Marekani waliouawa."

Ameongeza kuwa, "naamini kuwa wanaposema 'majeraha ya ubongo' ni nukta inayoashiria idadi ya wanajeshi waliouawa lakini hawataki kutangaza rasmi idadi hiyo."

Brigedia Shariff amesema kwa mujibu wa taarifa, makombora 13 ya Iran yaliyolenga kituo hicho yalisababisha hasara kubwa na kupelekea idadi kubwa ya wanajeshi wa Marekani kuangamizwa katika oparesheni hiyo.

Itakumbukwa kwamba tarehe 8 ya mwezi huu Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC lilitoa jibu kali ikiwa ni katika kujibu jinai za jeshi la Marekani baada ya kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha jeshi hilo la Iran. Katika jibu hilo IRGC ilishambulia kwa makombora kambi ya kijeshi ya Ain Assad ya Marekani nchini Iraq katika mkoa wa Al-Anbar.

Televisheni ya CNN juzi usiku ilitangaza habari kuhusu kuongezeka idadi ya wanajeshi wa Marekani waliojeruhiwa katika shambulio la Iran dhidi ya kambi ya kijeshi ya nchi hiyo ya Ain al Assad huko Iraq. CNN imewanukuu maafisa wawili wa Marekani na kutangaza kuwa hadi kufikia sasa wanajeshi wa Marekani wasiopungua 64 wamepata majeraha ya ubongo.

...........
340