Main Title

source : ParsToday
Jumapili

2 Februari 2020

07:54:29
1007084

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameutaja 'Muamala wa Karne' kama mpango wa Marekani wa kufedhehesha, aibu na wenye kuchukiza.

(ABNA24.com) Rais Rouhani amesema hayo leo Jumapili pambizoni mwa marasimu ya kuizuru Haram ya Imam Khomeini MA, Muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran viungani mwa Tehran ambapo ameongeza kuwa, njia pekee ya kukabiliana na wavamizi ni muqawama na umoja.

Amesema hii leo akthari ya watu duniani wamefahamu kuwa, mfumo wa Kiislamu ndiyo njia bora zaidi ya kufuata na wala sio sera za kujidhalilisha na kujitweza. Kadhalika amekosoa vikali sera ya madola ya kibeberu ya kuibua taharuki na migogoro.

Dakta Rouhani ameashiria kuhusu kujitokeza idadi kubwa ya watu katika mazishi ya Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) aliyeuawa kigaidi akiwa katika ziara rasmi nchini Iraq mapema mwezi uliopita wa Januari, na kueleza bayana kuwa, ushiriki huo uliidhihirishia dunia kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu yangali hai.

Rais Hassan Rouhani wa Iran ameandamana na mawaziri katika Haram ya Imam Rouhullah Khomeini kusini mwa Tehran kwa mnasaba wa kuanza maadhimisho ya 'Alfajiri Kumi' ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Maadhimisho hayo ya kihistoria yalianza rasmi jana Jumamosi tarehe 12 mwezi Bahman sawa na Februari Mosi, na katika kipindi cha siku kumi za mapinduzi ya miaka 41 iliyopita, taifa la Iran liliweza kupata ushindi licha ya uungaji mkono wa Marekani kwa utawala wa kidikteta wa Shah Pahlavi uliodumu kwa miaka 2,500.  

..........
340