Main Title

source : ParsToday
Jumatano

5 Februari 2020

08:22:09
1008027

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amekosoa kuhalifu ahadi kunakofanywa na Marekani na msimamo legevu unaoonyeshwa na Umoja wa Ulaya katika kukabiliana na Washington.

(ABNA24.com) Ali Larijani ameyasema hayo katika mazungumzo na Josep Borrell, Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya sambamba na kueleza utayari wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kusaidia kutatua matatizo ya kikanda.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika mjini Tehran hapo jana, Mkuu wa Sera za Nje wa EU alitoa mkono wa pole kwa Spika wa bunge la Iran kwa kuuliwa kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na akabainisha kuwa, Umoja wa Ulaya nao pia uko tayari kushirikiana na Iran kwa ajili ya kutatua masuala ya pande mbili na ya kieneo.

Jinsi ya kuyalinda makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, kupambana na ugaidi na kukabiliana na usambazaji wa mihadarati ni ajenda muhimu zaidi zilizotawala mazungumzo kati ya Larijani na Borrell.

Tangu alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, jana alifanya safari yake ya kwanza rasmi nchini Iran, ambapo kabla ya kukutana na Spika wa Bunge alifanya mazungumzo pia na Rais pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu.

...........
340