(ABNA24.com) Brigedia Jenerali Amir Hatami amesema hayo Jumanne hapa jijini Tehran na kufafanua kuwa, adui huko nyuma alikuwa akizungumza kwa majivuno kuhusu machaguo yake yaliko mezani hususan chaguo la kijeshi lakini hii leo, amefyata mdomo.
Amesema Marekani ilitekeleza na kukiri wazi wazi kuwa imefanya ugaidi wa kumuua Jenerali Soleimani, na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilitoa majibu mawili kwa chokochoko hizo; mosi jibu laini ambapo wananchi wa Iran walijitokeza kwa mamilioni katika kuuaga na kuuenzi mwili wa Shujaa huyo, na pili kwa jeshi la SEPAH kupiga kwa makombora kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq.
Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, "taifa hili halina haja ya kusema litachukua hatua gani iwapo maadui watafanya kosa, wenyewe wanafahamu vyema."
Brigedia Jenerali Amir Hatami ameongeza kuwa, katika hali ambayo adui hivi sasa anazungumza kuhusu mashinikizo ya juu ili kupunguza nguvu za Iran, lakini taifa hili linaendelea kuimarika na kuwa na uwezo mkubwa siku baada ya siku.
Ameeleza bayana kuwa, Iran imepiga hatua katika nyuga za nishati ya nyuklia, mafuta na uundaji magari na ndiposa maadui hivi sasa wanazuia chakula na dawa kuingia nchini ili kutoa pigo kwa wananchi wa Iran.
...........
340