Main Title

source : ParsToday
Jumatano

5 Februari 2020

08:22:10
1008030

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa Muamala wa Karne ni mchezo wa Marekani na utawala haramu wa Kizayuni kwa lengo la kuendelea kuwepo kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) kwa ajili ya kueneza chuki dhidi ya Uislamu.

(ABNA24.com) Shamkhani amesema hayo leo kupitia ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na kuongeza kuwa Muamala wa Karne bila shaka ni pigo kwa nchi za Kiislamu.

Aidha akiashiria vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa madhumuni ya kuudhoofisha muqawama na kuchochea chuki dhidi ya Tehran kuwa ni sehemu nyingine ya malengo ya Muamala wa Karne Shamkhani amesema kuwa, mpango huo ni vita vya niaba vya kujaribu kuzisambaratisha nchi zinazounga mkono muqawama.

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amefafanua kuwa licha ya kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC, lakini muqawama umeendelea kubakia hai kwa azma ya vijana wanamapinduzi wa Iran.

Hivi karibuni Rais Donald Trump wa Marekani akishirikiana na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Utawala Haramu wa Kizayuni walizindua mpango wa Muamala wa Karne.

Mpango huo unautambua mji wa Quds kuwa ni mji mkuu wa utawala khabithi wa Israel, kuukabidhi utawala huo asilimia 30 ya eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, kuwazuia wakimbizi wa Kipalestina kurejea katika nchi yao na kuizuia kikamilifu Palestina kuwa na silaha.

............
340