Main Title

source : ParsToday
Jumapili

9 Februari 2020

09:34:24
1008864

Ali Akbar Velayati, Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, Muamala wa Karne ni mpango wa kipumbavu kwani Wamarekkani wamefanya biashara na kitu ambacho siyo miliki yao.

(ABNA24.com) Ali Akbar Velayati amesema hayo mjini Qum hapa Iran katika shughuli ya Arubaini ya mashahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mhadi al-Mahandes waliouawa shahidi mwezi uliopita katika shambuulio la roketi la Marekani jirani na uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Baghdad.

Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, Wamarekani wanapaswa kutambua kwamba, wataondoka tu Iraq hasa kwa kuzingatia kuwa, taarifa zilizopo zinaonyesha kwamba, sehemu kubwa ya Bunge la Iraq inaunga mkono kufukuzwa wanajeshi wa Marekani katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Velayati ameyataka pia makundi yote ya Kipalestina kudumisha umoja na mshikamano baina yao ili yaweze kukabiliana na mpango khabithi na uliiojaa njama kama huu wa Muamala wa Karne.

Dakta Velayati ameongeza kuwa, hii leo kwa baraka za damu ya shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, zama za uwepo wa Marekani katiika eneo la Asia Magharibi zimefikia tamati.

Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema pia kuwa, Wamarekani walidhani kwamba, kwa kumuua Qassem Soleimani wangezima cheche za kambi ya muqawama, lakini mambo yamekuwa kinyume kwani mhimili wa muqawama umefikia katika kilele nchini Iran, Syria, Iraq, Lebanon na Palestina.

...........
340