Main Title

source : ParsToday
Jumatatu

10 Februari 2020

08:07:53
1009192

Maandamano makubwa ya 22 Bahman (11 Februari) katika kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yamepangwa kufanyika katika miji na vijiji 5,200 kote Iran.

(ABNA24.com) Hayo yamedokezwa na Nasrullah Lotfi, Kaimu Mkuu wa Baraza la Uratibu la  Shirika la Tablighi ya Kiislamu nchini Iran. Akizungumza na waandishi habari mjini Tehran leo Jumapili, amesema mwaka huu maadhimisho ya 22 Bahman yamepewa jina la 'Mapinduzi ya Kiislamu Yako Hai Katika Nuru ya Kumfuata Faqihi Mtawala, Jihadi na Mapambano (Muqawama)".

Ameongeza kuwa, maandamano ya mwaka huu yataakisiwa na waandishi habari elfu sita Wairani na wa kigeni ambao watakuwa katika maeneo yote ya Iran.

Nasrullah Lotfi ameongeza kuwa, sifa ya kipekee ya maadhimisho ya mwaka huu ni kumuenzi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye aliuawa shahidi Januari 3 katika hujuma ya kigaidi ya Marekani nchini Iraq. Aidha amesema Rais Hassan Rouhani atahutubu katika maadhimisho hayo ya 22 Bahman mjini Tehran siku ya Jumanne.

Aidha amesema kesho Jumatatu usiku kutasikika nara ya Allahu Akbar kote Iran ambapo kutakuwa na maonyesho ya fataki mjini Tehran na baadhi ya miji ya Iran katika mkesha wa 22 Bahman.

Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalifikia ushindi mnamo Februari 11 1979 (22 Bahman kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Shamsia) chini ya uongozi wa Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

.............
340