Main Title

source : ABNA
Jumanne

11 Februari 2020

16:38:57
1009481

habari za picha

Mjumuiko wa vijana wa Muqawamah kwa kumkumbuka Shahidi Qasim Soleimani na Abumahdi Muhandisi katika mji wa Qum

Shirika la Habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kufuatia mwaka wa kwanza wa kuasisiwa jumuia ya kimataifa ya vijana wa Muqawama ikiambatana na arubaini ya Shahidi Qasim Soleimani na Abumahdi Muhandisi, vijana wa Muqawama kutoka pande zote Duniani wamejumuika pamoja usiku wa Jumapili katika msikiti mkubwa wa sala ya Ijumaa katika mji mtakatifu wa Qum, mjumuiko ambao ulihudhuriwa na familia ya Shujaa kamanda Qasim Soleimani. Aidha katika mkusanyiko huu kamanda “Fadavi” ambaye ni naibu kamanda mkuu wa jashi la kulinda mapinduzi ya Iran, na Hujatul Islamu “Sayyed Hashim Safiyu Dini” walipata nafasi za kuzungumza katika mjumuiko huo, kwa upande mwingi mjumuiko huo ulihudhuriwa na Hujatul Islam “Muhsin Araki” na Sheikh Isa Qasim na baadhi ya viongozi wengine waliopata wasaa wa kushiriki katikja mjumuiko huo.