Main Title

source : ParsToday
Jumatano

12 Februari 2020

09:27:28
1009730

Mkuu wa Shirika la Atomiki la Iran amehutubu katika Kikao cha Kila Miaka Miwili cha Usalama wa Nyuklia mjini Vienna, Austria na kusema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitalegeza msimamo katika kulinda usalama wake.

(ABNA24.com) Ali Akbar Salehi, Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomikili la Iran aliyasema hayo jana Jumatatu na kuongeza kuwa : "Kulinda mapatano ya nyuklia ya JCPOA kutaweza kudhamini usalama wa nyuklia." Aidha amezikumbusha nchi za Ulaya kuhusu majukumu yao kama moja kati ya pande zilizoafiki mapatano hayo na kusema zinapaswa kuchukua hatua za kuyalinda na zijikwamue kutoka katika sera za utumiaji mabavu na za uchukuaji maamuzi ya upande mmoja za Marekani.

Hali kadhalika Salehi amesema serikali ya Marekani ndio mhusika mkuu wa hali mbaya iliyojitokeza huku akilaani sera zisizo za uwajibikaji na zisizo za kimantiki za utawala wa Marekani na utawala wa Kizayuni katika uwanja huo.

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema sera za Marekani katika uga wa kimataifa ni za kigaidi na amekumbusha pia kuhusu kuuawa kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema Iran iko tayari kutoa jibu kali kwa kila aina ya hujuma dhidi yake.

Salehi Aidha amekumbusha kuhusu hatua za uhasama dhidi ya Iran katika uga wa usalama wa nyuklia na kusema, jamii ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua za kukabiliana na vitisho vya mitandao ya intaneti kama vile kirusi cha Stuxnet ambacho kililenga vituo vya nyuklia vya Iran na pia ugaidi katika kuuawa shahidi wasomi wa nyuklia wa Iran.

...........
340