Main Title

source : ParsToday
Jumatano

12 Februari 2020

09:27:28
1009732

22 Bahman; kuwa pamoja wananchi wa Iran na Mapinduzi ya Kiislamu, siri ya kudumu mapinduzi haya

Jumanne ya leo iliyosadifiana na maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kwa mara nyingine tena wananchi wa Iran wamejitokeza kwa wingi katika matembezi ya maadhimisho ya miaka 41 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuonyesha mchango na nafasi yao athirifu kwa mapinduzi haya.

(ABNA24.com) Mahudhurio ya  daima ya wananchi wa Iran katika medani, ni moja ya sababu kuu za kudumu na kubakia Mapinduzi ya Kiislamu; na nguzo hii muhimu ndio inayoyatofautisha mapinduzi haya na mapinduzi mengine yaliyotokea katika pembe mbalimbali za dunia.

Mahudhurio athirifu ya wananchi wa Iran katika medani mbalimbali za Mapinduzi ya Kiislamu na kuwa kwao pamoja na mfumo wa Kiislamu wa Iran kumezifanya nguvu za Iran na uwezo wa kumfanya adui asithubutu kulishambulia taifa hili kuwa ni nguvu na uwezo unaotokana na wananchi. Mahudhurio haya ya wananchi kwa hakika yamesambaratisha njama na vitisho vya maadui ikiwemo Marekani.

Chuki na hasama za serikali mbalimbali zilizotawala nchini Marekani baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu dhidi ya wananchi wa Iran ni ithbati tosha kabisa kwamba, viongozi wa Washington wanachukizwa mno kuona wananchi wa taifa hili wapo pamoja na mapinduzi haya ya Kiislamu, kwani wananchi hawa wamekuwa kikwazo na kizingiti kikubwa kwa malengo yao machafu.

Baada ya kuingia madarakani Rais Donald Trump wa Marekani chuki na uadui wa Washington dhidi ya Iran uliongezeka zaidi na kivitendo serikali ya Trump sasa inawalenga moja kwa moja wananchi wa taifa hili.

Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, utawala wa Marekani umetumia mbinu mbalimbali kama ugaidi wa kiuchumi na wa kiserikali ili kuwatenganisha na mapinduzi wananchi wa Iran. Hata hivyo hatua ya wananchi wa Iran ya kuwa pamoja na Mapinduzi ya Kiislamu imekwamisha njama zote za serikali ya Washington.

Mahudhurio ya mamilioni ya wananchi katika shughuli ya kuuaga mwili wa shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH), yalionyesha kuwa, hata kwa kutumia mbinu kama za ugaidi wa kiserikali, Marekani haiwezi kuleta mfarakano katika jamii ya Wairani.

Katika uwanja huu, matokeo ya pekee ya risala muhimu ya kuuliwa kamanda wa kambi ya muqawama katika eneo la Asia Magharibi, ni kupaza kwa pamoja sauti ya takwa la wananchi la kufukuzwa wanajeshi wa Marekani katika eneo, ambapo katika siku za hivi karibuni chuki ya wananchi wa eneo dhidi ya Marekani imekuwa  dabali na maradufu.

Akizungumza Jumatatu ya jana katika hadhara ya mabalozi na wawakilishi wa nchi za kigeni walioko hapa mjini Tehran, Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kubainisha kwamba, ufahamu finyu au ghalati wa uhakika wa Iran ndilo chimbuko la kutekelezwa siasa hatari na kueleza kwamba, mahudhurio ya mamilioni ya wananchi katika shughuli ya kuuaga mwili wa shahidi Qassim Soleimani pamoja na mashahidi wenzake, yalibainisha wazi chuki ya wananchi wa Iran na wa eneo dhidi ya siasa za Marekani.

Mahudhurio yenye umaizi na ya daima ya wananchi wa Iran katika medani mbalimbali za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yakiwemo matembezi ya leo ya maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yanatuma risala kwa walimwengu hususan Marekani kwamba, Mapinduzi ya Kiislamu yana mtaji na rasilimali ya kijamii yenye uhakika ambayo iko katika kivuli chake yaani wananchi, kwani licha ya njama zote, lakini yanaadhimisha mwaka wa 41 tangu yalipopata uushindi mwaka 1979 kwa uongozi wa Imam Khomeini.

Hii hali ya kuwa pamoja na Mapinduzi ya Kiislamu ambayo kwa mara nyingine tena imejidhihirisha leo na itadhihirika tena siku kumi zijazo katika uchaguzi wa Bunge, inaonyesha kuwa, wananchi wa Iran watakuwa na upeo na mwelekeo wenye mwanga na nuru katika fremu ya taarifa ya "Hatua ya Pili ya Mapinduzi ya Kiislamu".

...........
340