Main Title

source : ParsToday
Jumatano

12 Februari 2020

09:37:33
1009737

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa kuuliwa kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani kamanda shahidi wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) kutazidisha azma na irada ya mhimili wa muqawama.

(ABNA24.com) Akizungumza na chombo cha habari cha Lebanon cha al Ahad, Muhammad Javad Zarif amemtaja Luteni Jenerali Qassem Soleimani kuwa ni dhihirisho la msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu katika eneo la magharibi mwa Asia na kuongeza kuwa: Ni madhara na pigo kubwa kwa eneo hili na kwa pande zote zinazopigania amani ulimwenguni kumpoteza Luteni Jenerali Soleimani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa, matukio yanayoshuhudiwa katika eneo hili baada ya kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Soleimani hususan huko Iraq na Syria yamezielekeza fikra za watu katika siasa za uharibifu za Marekani.   

Kuhusu mpango wa Muamala wa Karne; Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameeleza kuwa,  Rais Donald Trump wa Marekani na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Israel wameuzindua mpango huo kwa lengo la kupata ushindi katika uchaguzi na kusalia madarakani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema mpango huo ni muamala wa kibiashara kwa ajili ya kuimarisha mamlaka ya utawala ghasibu wa Kizayuni.

Zarif amesema kuwa Marekani siku zote imekuwa ikiikingia kifua Israel kuhusu suala la Palestina na haijawahi kushughulikia suala hilo kama nchi patanishi. Amesema, Wapalestina leo hii wamefikia natija kwamba Marekani haiwezi kuwa mpatanishi kuhusu suala linalohusu ardhi zao bali inaukingia kifua kupita kiasi utawala wa Kizayuni wa Israel.

...........
340