Main Title

source : ParsToday
Alhamisi

13 Februari 2020

07:11:51
1009993

Wamarekani hawajajua nafasi adhimu ya taifa la Iran katika kipindi chote cha miaka 41 iliyopita

Mamilioni ya wananchi wa Iran jana na katika maadhimisho ya kutimia mwaka wa 41 tangu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini walijitokeza kwa wingi katika miji na maeneo mbalimbali na kusisitiza tena udharura wa kuendelea kusimama kidete mbele ya njama za ubeberu wa kimataifa unaoongozwa na Marekani.

(ABNA24.com) Tarehe 11 Bahman mwaka 1357 (Februari 11, 1979) yaani miaka 41 iliyopita taifa la Iran lilifanikisha Mapinduzi ya Kiislamu bila ya kutegemea madola ya kigeni. Katika kipindi chote cha miaka 41 iliyopita Iran ya Kiislamu imekuwa ikikabiliana na maadui waliokula kiapo na yamini. Hapa linakuja swali kwamba, ni nini sababu ya uadui huo mkubwa? Ni kwa nini uhasama na uadui huo haujakoma na kumalizika?

Sababu kubwa ya uadui huo ni taathira kubwa za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika meneo ya nje ya mipaka ya Iran. Hii ina maana kwamba, mapinduzi hayo yalikuwa kigezo cha kufuatwa na kuigwa kilichoyapa mataifa mengine matumaini mema ya kujikomboa kutoka kwenye makucha ya tawala za kibeberu tangu mwanzoni mwa ushindi wake hapa nchini. Kwa msingi huo ilikuwa wazi kwamba, ushindi wa taifa kubwa la Iran na kumfukuza beberu Marekani hapa nchini, ilikuwa hatua isiyoweza kuvumilika. Hivyo, Marekani na maadui wengine wa Mapinduzi ya Kiislamu walifanya kila waliloweza ili asaa wakafanikiwa kurejesha hali iliyokuwepo hapa nchini kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Swali jingine linalojitokeza ni kwamba, ni kwa nini Marekani na maadui wengine wa taifa la Iran hawakuweza kufikia malengo yao katika kipindi chote cha miaka 41 iliyopita?

Jibu la swali hilo limetolewa katika hotuba ya Rais Hassan Rouhani kwenye kilelel cha maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi hiyo jana mbele ya mamilionii ya wananchi. Dakta Rouhani alisema: Njia yetu ni kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa nchi hii.

Kwa sababu hiyo unaona kuwa, katika kipindi chote cha miaka 41 iliyopita kumejitokeza uadui na vinyongo vingi na kwa sura mbalimbali lakini Mapinduzi yameendeleza njia yake ya awali. Rais Rouhani ameongeza kuwa: "Kinachoyaimarisha zaidi Mapinduzi ya Kiislamu ni rai na mahudhurio makubwa ya wananchi." Vilevile amekumbusha kwamba katika kipindi chote hicho Marekani imefanya makosa makubwa.

Miongoni mwa makosa na jinai kubwa za Marekani ni mauaji yake ya kigaidi dhidi ya aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi al Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Luteni Jenerali Qassem Soleimani akiwa ugenini nchini Iraq. Baada ya mauaji hayo mamilioni ya wananchi wa Iran walimiminika mitaani kuuaga mwili wa shujaa huyo, suala ambalo pia limewaacha bumbuazi maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Kamanda Suleimani anajulikana sana baina ya watu wa nchi za Iraq, Syria na Lebanon kutokana na mchango wake mkubwa katika kuliangamzia kundi la kigaidi la Daesh.

Tangu mwanzoni mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu Wamarekani walitumbukia katika makosa ya kimahesabu. Makosa hayo yametokana na sababu mbili kuu: Kwanza ni kupuuza umuhimu wa masuala ya komaanawi na kiroho. Na pili ni kwamba adui Mmarekani bado hajawajua vyema wananchi wa Iran. Makosa kama haya makubwa yanaweza kuifanya nguvu kubwa kugonga mwamba na kushindwa. Makosa kama haya sambamba na kusimama kidete kwa taifa la Iran mkabala wa Marekani katika kipindi chote cha miaka 41 ndiyo yanayoifanya Marekani indelea kugonga mwamba na kuangukia pua.  

Mienendo ya kijinga ya Donald Trump mkabala wa Iran imethibitisha tena jinsi kiongozi huyo wa Marekani asivyoelewa vyema historia ya huko nyuma na ya sasa ya Marekani na Iran. Katika kipindi cha utawala wa Barack Obama ambaye alificha ngumi ya chuma kwenye glovu ya mahameli na kuzungumzia mageuzi katika siasa za Washington, Iran haitetereshwa na maneno hayo ya hadaa, iweje hii leo itishike kwa bwabwaja za Donald Trump?

Jumatatu iliyopita wakati Rais Hassan Rouhani alipokutana na mabalozi na wawakilishi wa nchi za kigeni na jumuiya za kimataifa waliopo Tehran kwa mnasaba wa maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema: Wale wanaojua vyema historia, ustaarabu na utamaduni wa Iran wanaelewa kwamba, Wairani kamwe hawatasalimu amri mbele ya sera za kutumia mabavu, maneno yasiyo ya haki na mashinikizo.

............
340