Main Title

source : ABNA
Ijumaa

14 Februari 2020

08:54:32
1010173

Barabara za Kaskazini na Kusini mwa Italy zapambwa kwa picha za Shujaa kamanda Qasem Soleimani

Shirika la Habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari makini kutoka Italy zinaeleza kuwa barabara mashuhuri za miji mikubwa ya Italy ikiwemo mji wa Rome na Milan, imepambwa na mamia ya mabango yenye picha za Kamanda Shujaa Qasim Soleimani.

Hatua hiyo imechukuliwa na kikundi cha mapambano cha Ulaya kwa kuikomboa Syria, ambapo katika ripoti ziliotolewa katika suala hili ni kwamba: malengo ya hatua hiyo ni kilichotajwa kuwa ni kumshukuru Shujaa aliyekuwa na ubinadamu mwenye kujitolea kwaajili ya uhuru wa mataifa mbalimbali ulimwenguni, ambapo mamilioni ya wanawake na wanaumi ulimwenguni wameathiriwa na ubinadamu na kujitolea kwake, wanaharakati wa Italy wamemtaja Shujaa Kamanda Qasem Soleimani kuwa ni Kamanda aliokuwa na imani ya hali ya juu, myenyekefu, ambaye hakuwahi kuchoka katika kukabiliana na mabeberu na wakandamizaji wa ulimwenguni, huku wakisistiza kuwa mauaji ya kamanda huyo ni jambo la unyama ukatili kilichokuwa kinyume na sheria.

MWISHO/290