Main Title

source : ParsToday
Jumamosi

15 Februari 2020

08:16:40
1010391

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah amefanya mazungumzo na televisheni ya al Mayadeen akieleza mchango na nfasi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuunda harakati hiyo ya mapambano na mafanikio ya Kamanda Qassem Soleimani.

(ABNA24.com) Nukta ya kwanza iliyoashiriwa katika matamshi ya Sayyid Nasrullah ni kwamba, kimsingi Hizbullah na muqawana ni kikosi cha kujihami kilichoanzishwa kwa ajili ya kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel, na mbali ya kuwa haina nia ya kupanua satua na ushawishi wake katika ulimwengu wa Kiarabu wala haipingani na nchi za Kiislamu na Kiarabu, inafanya jitihada za kulinda ardhi za nchi zote za Kiislamu na Kiarabu.

Hatakati ya Hizbullah ya Lebanon ilianzishwa baada ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuishambulia Lebanon mwaka 1982 na kukaribia kuuteka mji mkuu wa nchi hiyo, Beirut.

Nukta ya pili ni kwamba, Israel daima imekuwa ikitumia vibaya migogoro inayotokea katika uhusiano wa nchi za Waislamu. Katika mkondo huo vita vya Iraq dhidi ya Iran ilikuwa fursa kubwa kwa utawala huo ghasbu kwa ajili ya kuishambulia ardhi ya Lebanon na kujitanua zaidi. Hii leo pia utawala huo unatumia vita vya ndani na hitilafu, mizozo na migawanyiko baina ya nchi za Waislamu kwa ajili ya kuendeleza malengo yake ikiwa ni pamoja na kutekeleza njama iliyopewa jina la "Muamala wa Karne".

Sehemu nyingine muhimu mazungumzo ya Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon na televisheni ya al Mayadeen ni sisitizo lake kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haina mtazamo wa kimakundi na kimadhehebu kuhusiana na matukio ya ulimwengu na Umma wa Kiislamu na kwamba, inaamiliana na masuala hayo kwa mtazamo wa Kiislamu.

Amesisitiza ukweli huo kwa kusema kuwa, tangu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haikusita hata kidogo kutoa misaada ya aina mbalimbali kwa makundi na nchi za Kiislamu bila ya kujali madhehebu zao. Amesema Iran ya Kiislamu iliendelea kuisaidia Lebanon kwa hali na mali kwa ajili ya kukabiliana hujuma ya utawala haramu wa Israel licha ya kuwa katika vita vya kutwishwa vya miaka 8.

Akizungumzia shakshaia ya Shahidi Qassem Soleimani aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds ch Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Sayyid Hassan Nasrullah amesema Shahidi Soleimani alikuwa na mtazamo wa kidugu kwa wapiganaji wa Jihadi wa Lebanon na kwamba mtazamo huo ulijenga uhusiano wa kidugu baina ya kamanda huyo na wapiganaji wa Hizbullah.

Sayyid Nasrullah amesema: "Uhusiano kama huu ulisaidia sana kukutanisha pamoja mitazamo, mawazo, mipango, ushirikiano na jinsi ya kuvuka matatizo au hitilafu zozote zilizotazamiwa kujitokeza.” Kwa hakika mwenendo huu wa Al Haj Qassem Soleimani unathibitisha kuwa, mantiki ya Iran kuhusiana na suala la kuwepo udugu baina ya mataifa na nchi za Waislamu si nara tupu bali ni mwenendo unaotekelezwa kivitendo.

Sifa nyingine muhimu ya Shahidi Soleimani likuwa mahudhurio yake makubwa kaika medani za Jihadi na vita na ilikuwa mara chache sana Shahidi Soleimani kuonekana Tehran. Kuwepo kwake daima katika medani ya vita na Jihadi ilikuwa miongoni mwa sababu za kujenga uhusiano mkubwa na wa karibu na wanamapambano katika medani ya Jihadi.

Sayyid Hassan Nasrullah anasema, kutochoka na kuwa tayafi kukabiliana na hatari za aina mbalimbali ni miongoni mwa sababu za mafanikio ya Al Haj Qassem Soleimani. Katibu Mkuu wa Hizbullah anamalizia kwa kusema: “Moja kati ya neema kubwa sana za Mweyezi Mungu kwangu mimi katika maisha yangu ni kujuana na Al Haj Qassem Soleimani na udugu na urafiki liokuwepo baina yetu, ingwa neema zote za Mwenyezi Mungu kwangu mimi ni kubwa na adhimu.”  

...........
340