Main Title

source : ParsToday
Jumamosi

15 Februari 2020

08:16:41
1010392

Marasimu ya maombolezo ya 40 ya shahidi Luteni Jenerali Soleimani yafanyika kote nchini Iran

Marasimu ya maombolezo ya arubaini ya shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Qods cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ( SEPAH) yamefanyika leo kote nchini Iran kwa kuhudhuriwa na umati mkubwa wa matabaka mbalimbali ya wananchi.

(ABNA24.com) Kamanda shahidi Qassem Soleimani ambaye tarehe Tatu Januari mwaka huu alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo aliuliwa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq al Hashd al Sha'abi na wanajihadi wengine wanane katika shambulio la kigaidi la wanajeshi magaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad.  

Wananchi katika Iran nzima ya Kiislamu wameshiriki kwenye marasimu ya mombolezo ya arubaini ya shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na wanajihadi wenzake wengine na kusisitiza kuondoka wanajeshi magaidi wa Marekani katika eneo.

Matabaka mbalimbali ya wananchi hapa nchini zikiwemo familia za mashahidi, baadhi ya maafisa wa serikali na jeshi pia walifika katika haramu tukufu za Imam Reza (a.s) huko Mash'had na kwa Bi Fatima Maasuma (s.a) katika mji mtukufu wa Qum na kuomboleza kifo cha shahidi Qassem Soleimani.

Marasimu ya arobaini ya Kamanda Soleimani na wanajihadi wenzake yatafanyika  leo usiku  hapa Tehran pia kwa kuhudhuriwa na wageni kutoka nje ya nchi.

Wananchi katika miji mingine ya Iran ikiwemo Urumiye, Isfahan, Ilam, Mahabad, Ardabil, Birjand, Zahidan, Kerman, Shahr Kurd, Tabriz na Hamedan wamefanya kumbukumbu hii ya arobaini ambapo mbali ya kushukuru jibu kali lililotolewa na jeshi la Sepah kwa jinai za kigaidi za Marekani wamesisitiza juu ya kukabiliana vikali na njama zozote za Marekani katika eneo.

.............
340