Main Title

source : ParsToday
Jumamosi

15 Februari 2020

08:16:47
1010393

Salami: Shahidi Soleimani ni mhuishaji wa jihadi na shahada katika ulimwengu wa Kiislamu

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amemtaja Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha SEPAH kama shakhsia aliyehuisha 'harakati za jihadi na kuuawa shahidi' katika ulimwengu wa Kiislamu.

(ABNA24.com) Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema hayo jana usiku hapa Tehran aliposhiriki marasimu ya arubaini ya Kamanda Soleimani na Mashahidi wenzake na kusisitiza kuwa, "Jenerali Soleimani alikuwa mwenye huruma kwa watu, lakini mkali kwa maadui."

Ameeleza bayana kuwa, Shahidi Soleimani alitambua vyema umuhimu wa jihadi na alienda sehemu mbalimbali alikosikia watu wanadhulimiwa, na kwa msingi huo jenerali huyo ni kiigizo chema cha kufuatwa katika kuwalinda na kuwatetea Waislamu.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mara nyingine tena ameonya kuwa, jeshi la SEPAH halitasita kutoa pigo kwa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel iwapo zitachukua hatua yoyote ya kipumbavu dhidi ya taifa kubwa la Iran.

Kadhalika ametoa onyo kwa waitifaki wa utawala wa Marekani ambao ni adui wa umma wa Kiislamu na kusema kwamba, wanapaswa kusitisha njama zao ili wasiwe waathirika wa sera mbovu za Washington.  

Meja Jenerali Salami ameongeza kuwa, mrengo wa muqawama na mapambano ya Kiislamu una azma imara ya kuendeleza mapambano yenye malengo matakatifu na kwamba mustakabali utakuwa mwema kwani kumalizika uwepo wa Marekani ni jambo ambalo litaleta  uthabiti, ustawi, usalama na mlingano katika eneo la Asia Magharibi.

...........
340