Main Title

source : ParsToday
Jumamosi

15 Februari 2020

08:16:48
1010394

Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa Tehran amesema mpango wa 'Muamala wa Karne' ni fedheha kubwa na kashfa kwa Rais Donald Trump wa Marekani.

(ABNA24.com) Hujjatul Islam wal Muslimin Kadhim Siddiquie, katika hotuba zake wakati wa Sala ya Ijumaa Tehran amesema: Mpango wa 'muamala wa karne' umeibua mwamko na mapinduzi mapya katika ulimwengu wa Kiislamu na nukta hiyo itapelekea malengo machafu ya mpango huo wa Marekani-Kizayuni kugonga mwamba.

Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesisitiza kuwa, rais wa Marekani asiye na murua amepeana makazi ya Wapalestina kupitia 'mpango wa karne' katika hali ambayo mpango huo tayari umeshafeli.

Ikumbukwe kuwa, Jumanne ya tarehe 28 Januari, Rais wa Marekani, Donald Trump alizindua mpango wa Muamala wa Karne akiwa pamoja na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu.

Kwa mujibu wa mpango huo wa Marekani, Quds Tukufu itakabidhiwa kwa utawala wa Kizayuni; wakimbizi wa Kipalestina hawatakuwa na haki tena ya kurejea katika ardhi za mababu zao na Palestina itamiliki tu ardhi zitakazosalia huko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Gaza.

Kwingineko katika hotuba yake, Hujjatul Islam wal Muslimin Kadhim Siddiquie ameashiria uchaguzi ujao wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, na kusema bunge lijalo linapaswa kuwa na wajumbe wanaowapenda wananchi na liende sambamba na damu ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, IRGC, aliyeuawa shahidi katika hujuma ya kigaidi ya Marekani mwezi uliopita wa Januari.

Uchaguzi wa Bunge la Iran utafanyika Ijumaa Februari 21 2020.

............
340