Main Title

source : ParsToday
Jumapili

16 Februari 2020

08:18:10
1010740

Udharura wa kushikamana Waislamu, mhimili wa muqawama katika kuwafukuza wanajeshi wa Marekani Asia Magharibi

Hii leo mhimili wa muqawama si Iran pekee bali umeenea kuanzia Bahari Nyekundu hadi ya Meditarania na kuanzia Harakati ya Ansarullah ya Yemen hadi Hizbullah ya Lebanon.

(ABNA24.com) Ukweli huo wa mambo umebainishwa na Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) wakati alipohojiwa na televisheni ya al Masira ya Yemen na kuongeza kuwa: nchi zote za Kiislamu na mhimili wa muqawama zinapasa kushikamana na kuwa kitu kimoja ili kuwafukuza wanajeshi wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi.  

Harakati za muqawama huko kusini mwa Lebanon siku zote zimekuwa zikikumbushia mapambano na vita dhidi ya Wazayuni maghasibu; mapambano ambayo yanaendelea hadi sasa tangu mwaka 1982. Kukimbia kwa madhila utawala wa Kizayuni huko Lebanon mwaka 2000 Miladia, vipigo ilivyopata Israel katika vita vya siku 33 huko Lebanon mwaka 2006, vita vya siku 22 huko Ghaza mwaka 2009 na vile vya siku 51 vya Ghaza pia mwaka 2014 ni miongoni mwa mafanikio makubwa ya harakati ya muqawama huko Lebanon na Palestina.

Wakati vilipotokea vita vya siku 33 huko Lebanon aghalabu ya wachambuzi wa mambo walizungumzia ushindi mkubwa ilioupata harakati ya muqawama katika vita hivyo na kukiri kwamba sasa umefika wakati wa kubadilishwa mlingano wa nguvu katika eneo hili.

Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi  alisema katika ujumbe wake kwa wananchi wa Lebanon kufuatia ushindi uliopatikana katika vita hivyo alisema kuwa: "Lebanon imeng'aa kwa baraka na ushujaa wa wananchi wake. Adui alikosea kwa kudhani Lebanon  ni nchi dhaifu zaidi katika eneo hili na hivyo ataweza kutekeleza mpango wake mchafu wa Mashariki ya Kati kwa kuishambulia nchi hiyo. Taifa la Lebanon na vijana wake jasiri na wanasiasa wenye vipawa wamemtoa adui kwa nguvu katika dimbwi la mghafala wake huo.

Moja ya ishara za wazi kabisa za kufeli huko adui, ni kusambaratika hali ya kujiamini ya jeshi la utawala wa Kizayuni; jeshi ambalo lilikuwa likijigamba kuwa halishindiki kabisa.  

Ukurasa mpya wa nguvu za kambi ya muqawama ulifunguliwa tarehe 8 Januari mwaka huu wakati Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) lilipoitwanga kwa makombora 13 kambi ya kijeshi ya Marekani ya Ain al Asad mkoani al Anbar magharibi mwa Iraq ikiwa ni katika kujibu jinai za jeshi la Marekani la kumuuwa kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la SEPAH na wanajihadi wenzake tisa karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad.

Jibu la kwanza la Iran kwa wanajeshi magaidi wa Marekani katika eneo limewapelekea wachambuzi wa kistratejia kuwaslisha nadharia mpya kuhusu uwezo wa harakati ya muqawama mbele ya vikosi vamizi katika eneo la Asia Magharibi. Nadharia hizo zimepelekea kukubaliwa ukweli huu kwamba leo hii mhimili wa muqawama ni moja ya pande kuu zlizo na mchango na nafasi athirifu katika eneo. Kushindwa pakubwa magaidi wa Daesh huko Iraq, ushindi mtawalia wa muqawama huko Syria na ushindi wa harakati ya Ansarullah huko Yemen ni miongoni mwa matunda muhimu na makubwa ya muqawama katika eneo hili.

Ibrahim Muhammad al Dulaimi Balozi wa Yemen nchini Iran amesisitiza katika Mkutano wa Kimataifa uliofanyika juzi Alkhamisi chini ya anuani " Shahidi Soleaimani, Jiografia ya Muqawama na Usalama wa Dunia kwamba kuna udharura wa kushikamana barabara mhimili wa muqawama na kueleza kuwa: Mashambulizi ya makombora ya Iran katika kambi ya kijeshi ya Marekani ya Ain al Asad yalikuwa pigo kubwa kwa Wamarekani na vibaraka wao na kwamba wanamuqawama watafanya kazi zaidi na yenye taathira kubwa zaidi na watadhihirisha kivitendo kwamba taathira za kambi ya muqawama hazimithiliki.  

Ukitazama kwa ufupi ripoti na uchambuzi wa Taasisi za Utafiti za Think Tanks utaona kuwa nafasi ya muqawama katika eneo la Asia Magharibi leo hii ni yenye athari kubwa isiyokanushika.  Hapana shaka kuwa nafasi ya mashahidi adhimu kama Luteni Jenerali Qassem Soleimani daima itaendelea kuenziwa; na harakati hii haitasita hadi yastakapotimia malengo yake ya kupambana na uistikbari na kuwafurusha wanajeshi vamizi katika eneo hili.

Katika makala yake maalumu ya mwaka, jarida la Foreign Policy la nchini Marekani limemtaja Luteni Jenerali shahidi Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) kuwa mmoja kati ya shakhsia kumi adhimu kwenye nyanja za kiulinzi, kiusalama na kimuqawama katika mwaka uliopita wa 2019 duniani.   

Hapana shaka kuwa kile kilichotokea katika eneo hili baada ya jinai ya hivi karibuni ya Marekani ya kumuuwa kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani ni kumalizika awamu moja na kuanza awamu nyingine mpya kwenye njia ya ushindi. Katika awamu hii, umoja wa nchi za Kiislamu na wanamuqawama ni mambo yatakayotoa taathira muhimu kwa mustakbali wa Palestina ambayo ndiyo kadhia yenye umuhimu mkubwa zaidi kwa ulimwengu wa Kiislamu na kufelisha njama za kishetani za Trump alizozipachika jina la Muamala wa Karne.

............
340