Main Title

source : ParsToday
Jumatano

19 Februari 2020

07:45:07
1011583

Wendy Sherman, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Marekani ameitaja jinai ya serikali ya Trump ya kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, kuwa ni hatua yenye hatari kubwa.

(ABNA24.com) Sherman aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje katika serikali ya Barack Obama amesema kuwa, Trump ametekeleza maafa katika sekta nyingi na kwamba kumuua kigaidi Luteni Soleimani ni hatua iliyojaa hatari kwani imeziweka Iran na Marekani katika mstari wa makabiliano ya vita.

Ameongeza kuwa hatua ya serikali ya Trump ya kumuua kamanda huyo mkubwa wa Iran, iliibua radiamali kubwa miongoni mwa raia wa Iran suala ambalo ni kwa madhara ya Marekani. Itakumbukwa kuwa Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aiyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC na Abu Mahdi al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Iraq Hashdu sh-Sha'abi na shakhsia wanane wengine walioandamana nao waliuawa usiku wa tarehe 3 Januari karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad, Iraq.

Kufuatia jinai hiyo Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC lilitoa jibu kali kwa kushambulia kwa makombora zaidi ya 10 kambi ya kijeshi ya Marekani ya Ain Assad katika mkoa wa Al-Anbar hapo tarehe 8 Januari mwaka huu.

Baada ya shambulizi hilo Trump alidai kuwa hakukuwa na mtu aliyeuawa wala kujeruhiwa katika operesheni hiyo ya Jeshi la IRGC. Hata hivyo siku chache baadaye Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) iliendelea kutoa taarifa za idadi ya askari wa nchi hiyo waliojeruhiwa katika shambulizi hilo. Katika taarifa ya mwisho ya Pentagon, hadi sasa askari 109 wa Marekani walijeruhiwa kiubongo katika jibu hilo la makombora la Iran.

.............
340