Main Title

source : ABNA
Alhamisi

20 Februari 2020

07:08:56
1011805

Maadhimisho ya miaka 41 ya mapindunzi ya Iran pamoja na siku ya Arubaini ya kuuwawa kamanda Soleimani na Muhandisi nchini Ghana

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: maadhimisho ya sherehe ya kukumbuka za miaka 41 ya mapinduzi ya kiislamu ya Iran ikiambatana na arubaini ya Shahidi kamanda Qasim Suleimani na Abumahdi Almuhandisi pamoja na waliokuwa pamoja nao, yamefanyika nchini Ghana katika mji mkuu wa nchi hiyo. Maadhimisho hayo ylihudhuriwa na msafara wa jumuia ya kimataifa ya AhlulBayt (a.s) iliofanya safari nchini humo. kwa upande mwingine zidi ya 400 kutoka madhehebu, makabila, viongozi wakubwa wa mji na maimamu wa sala za Ijumaa, viongozi wa kisiasa na jumuia za wanawake walijumuika pamoja katika maadhimisho hayo na kutoa pongezi za miaka 41 ya mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Hujatul-islamu “Muhammad Ali Muinioni”, Sayyed Zamani Huseini, ni katika watu waliozungumza katika maadhimisho hayo.