Main Title

source : ParsToday
Jumatatu

24 Februari 2020

08:07:22
1012814

Sisitizo la Kiongozi Muadhamu kuhusu udharura wa kuwa macho mbele ya njama za maadui na kuwa tayari kutoa jibu na pigo mkabala

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amewashukuru wananchi kwa kuufuzu kwa kiwango cha kuridhisha mtihani mkubwa wa uchaguzi na kuweza kuzima propaganda za kila upande za maadui na kutumia kwao vibaya suala hilo na akasisitiza kwamba: Taifa zima linapaswa kuwa macho na kujiweka tayari kukabiliana na njama za adui zinazolenga kutoa pigo kwa mihimili tofauti ya nchi.

(ABNA24.com) Ayatullah Khamenei aliyasema hayo Jumapili asubuhi mjini Tehran katika utangulizi wa darsa ya marhala ya juu kabisa ya fiqhi. Ameashiria propaganda kubwa na za sumu za vyombo vya propaganda vya maajinabi za kuwashawishi wananchi wasishiriki katika uchaguzi; na akasema: Propaganda hizo hasi zilianza tangu miezi kadhaa nyuma na zikaongezeka wakati wa kukaribia uchaguzi; na katika siku mbili za mwisho na kwa kisingizio cha kuzuka kirusi na maradhi fulani, vyombo hivyo vya habari havikuacha kutumia kila fursa viliyopata kuwashawishi wananchi wasishiriki katika uchaguzi.

Kiongozi Muadhamu ameashiria namna maadui wanavyohasimiana na taifa la Iran na kusema uhasama huo hauishii tu katika nyuga za uchumi, utamaduni, itikadi za kidini na kimapinduzi za wananchi na kuongeza kuwa:  Wao wanapinga hata uchaguzi wa taifa la Iran, kwa sababu hawataki ithibitike hakika ya ushiriki wa wananchi  katika uchaguzi kwa jina la dini na upigaji kura wao kwa ajili ya Mapinduzi.

Ayatullah Khamenei amesema, kufanyika uchaguzi katika Mfumo wa Kiislamu kunabatilisha madai ya maadui kwamba dini inapingana na uhuru na demokrasia; na akabainisha kuwa: Uchaguzi katika Jamhuri ya Kiislamu unaonyesha kwamba dini ni dhihirisho kamili la demokrasia ya pande zote; na kufanyika chaguzi 37 ndani ya muda wa miaka 41 kunaonyesha umuhimu usio na kifani unaotoa Mfumo wa Kiislamu kwa nafasi ya chaguo la wananchi.

Katika miaka yote baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Marekani imekuwa ikilenga kudhoofisha mfumo wa Kiislamu na kuvuruga umoja wa taifa la Iran sambamba na kutekeleza njama ya kuibua hitilafu na migawanyiko ya kisiasa ndani ya jamii ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Lakini kuwa macho taifa la Iran mbele ya harakati za kuvuruga hali ya mambo, kama ilivyoshuhudiwa katika uchaguzi wa bunge, ni jambo ambalo limepelekea adui asiweze kujipenyeza.

Hotuba ya jana ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ilikuwa na nukta mbili muhimu.

Kwanza ni umuhimu wa kushiriki kwa wakati wananchi katika lahadha hasasi jambo ambalo limewasambaratisha maadui na hivyo kuonyesha uwezo wa pande zote wa taifa la Iran.

Kwa mtazamo wa weledi wa mambo, propaganda za Marekani dhidi ya Iran ni sehemu ya vita laini ambapo mbinu ambayo imekuwa ikitumiwa ni kujaribu kudunisha ushiriki wa wananchi katika uchaguzi. Hata hivyo njama hiyo iliyoratibiwa imegonga mwamba na kufeli.

Nukta ya pili ni kuwa; katika hotuba yake, Kiongozi Muadhamu amesisitiza juu ya utayarifu unaozidi kuimarika wa wananchi kwa ajili ya kutoa jibu mkabala kwa adui mvamizi.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa wito kwa wananchi wote kumtambua vyema adui na kuwa macho katika kukabiliana naye, na akasisitiza kwamba: Katika kukabiliana na harakati za maelfu ya watu wanaotumikia kambi ya adui dhidi ya masuala mbali mbali ya Iran, inapasa wawepo mamilioni ya watu katika kambi ya Iran waliojiandaa kwa ajili ya kulinda na kutoa mapigo mkabala katika masuala ya uenezi na kazi mbali mbali zinazoweza kufanywa kwa ajili ya taifa.

Tokea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979, maadui wamekuwa wakitumia kila mbinu kutoa pigo kwa mfumo wa Kiislamu lakini leo wamejikita zaidi katika kubadilisha sera au msimamo wa mfumo na kudhoofisha uwezo wa kujihami Iran.

Ili kutoa pigo kwa Iran, Marekani imechukua hatua kadhaa lakini kila mara hupigwa kibao na taifa la Iran. Mnamo 3 Januari 2020, katika hatua ya kigaidi, Marekani ilitekeleza kitendo cha ugaidi wa kiserikali kwa kumuua Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu pamoja na watu aliokuwa ameandamana nao. Shahidi Soleimani alikuwa Iraq kwa mwaliko rasmi wa serikali ya Iraq. Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika kujibu jinai hiyo, mnamo Januari 8 lilivurumisha makombora 13 ya balistiki katika kambi ya kijeshi ya Ainul Assad ya Jeshi la Marekani katika mkoa wa Al Anbar nchini Iraq.

Uzoefu unaonyesha kuwa, wananchi wana nafasi muhimu na ya kudumu katika kudhihiri nguvu na uwezo wa Iran. Kwa hakika uwajibikaji wa wananchi na kujitokeza kwa wakati katika medani ni jambo ambalo limemsambaratisha adui na kubadilisha vitisho kuwa fursa kwa jili ya kunawiri uwezo wa taifa la Iran.

..........
340