Main Title

source : parstoday
Jumamosi

11 Aprili 2020

06:59:42
1024325

Ismail Haniya: Siasa za mauaji za Marekani na Israel zimeongeza nguvu ya kambi ya muqawama

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa, siasa za Wazayuni za kuwaua viongozi wa muqawama na mauaji yaliyofanywa na Marekani dhidi ya Luteni Jenerali Qassim Soleimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) hazijakuwa na natija nyingine ghairi ya kuongeza nguvu na adhama ya kambi ya muqawama.

(ABNA24.com) Ismail Haniya amesema hayo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Ayatullah Ibrahim Raeisi, Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran ambapo sambamba na kushukuru himaya na uungaji mkono wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na taifa la Iran kwa wananchi wa Palestina na Gaza amesema kuwa, uungaji mkono huu ni ishara ya dhamira zilizo macho na zenye welewa za taifa la Iran.

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa ameashiria siasa za muaji za Wazayuni dhidi ya viongozi wa muqawama na kubainisha kwamba, siasa hizo hazitakuwa na natija nyingine ghairi ya muqawama kuzidi kuwa na nguvu, kutimuliwa wavamizi kutoka katika ardhi za Palestina na kurejea wakimbizi katika ardhi za mababu zao.

Haniya amesisitiza pia kuwa, muqawama na mapambano ya wananchi madhulumu wa Palestina yataendelea mpaka pale yatakapopata ushindi dhidi ya Wazayuni maghasibu na kuachiliwa wafungwa wote wa Kipalestina kutoka katika magereza ya Israel.

Kwa upande wake, Ayatullah Ibrahim Raeisi, Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran ameashiria masaibu wanayopata wananchi wa Gaza kutokana na mzingiro wa Israel pamoja na dhulma wanayotendewa Wapalestina na kusisitiza juu ya udharura wa kuachiliwa huru mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za utawala ghasibu wa Israel.

............
340