Main Title

source : parstoday
Jumapili

12 Aprili 2020

18:45:12
1024946

Nigeria yatakiwa kumwachia huru Sheikh Zakzaky wakati huu wa corona

Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) imetoa mwito wa kuachiwa huru kiongozi wake, Sheikh Ibrahim Zakzaky anayekabiliwa na hatari ya kuambukizwa virusi vya corona akiwa kizuzini.

(ABNA24.com) Katika taarifa, IMN imemhutubu Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo na maafisa wa serikali katika jimbo la Kaduna ikitaka mwanachuoni huyo wa kidini aachiwe huru mara moja. Taarifa hiyo imesema, "Sheikh Zakzaky anapaswa kuwa huru kutokana na sababu nyingi hususan wakati huu ambapo taifa linakabaliana na janga la virusi vya corona."

Taarifa ya Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imekumbusha kuwa, hata kabla ya mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 (corona), kiongozi huyo wa kidini alitakiwa kuachiwa huru kutokana sababu za kiafya.

Nigeria imethibitisha kuwa na kesi zaidi ya 250 za wagonjwa wa Covid-19 huku virusi hivyo angamizi vikiua watu saba kufikia sasa katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Februari mwaka huu, Mahakama ya Nigeria iliakhirisha tena kusikiliza kesi ya Sheikh Zakzaky, na kusema kuwa itasikilizwa tarehe 23 na 24 Aprili mwaka huu.

Licha ya Mahakama Kuu ya Nigeria kuwahi kutoa hukumu iliyosisitiza kuwa Sheikh Zakzaky pamoja na mkewe hawana hatia yoyote na ikaamuru waachiliwe huru, lakini wawili hao wangali wameendelea kuwekwa jela licha ya hali zao za afya kuwa mbaya sana, tangu walipotiwa nguvuni mwaka 2015 baada ya jeshi la Nigeria kushambulia Husainia ya mji wa Zaria jimboni Kaduna.

............
340