Main Title

source : parstoday
Jumatano

15 Aprili 2020

06:21:59
1025967

Marasimu ya kukumbuka siku 100 tokea kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC pamoja na Abu Mahdi al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Hashdu sh-Sha'abi ya Iraq, zimefanyika mjini Karbala nchini humo.

(ABNA24.com) Itakumbukwa kuwa shahidi Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandis waliuawa tarehe tatu Januari mwaka huu, katika shambulii la kigaidi lililotekelezwa na askari magaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa mjini Baghdad, Iraq.

Mtandao wa habari wa Harakati ya Wananchi ya Hashdu sh-Sha'bi, umetangaza kuwa, kutokana na kuenea virusi vya Corona, kumbukumbu hiyo ilifanyika Jumatatu kwa njia ya video.

Aidha umeongeza kuwa, katika marasimu hayo ambayo yalifanyika bila kuhudhuriwa na watu kwa njia ya kawaida, kulitolewa heshima kwa picha za  mashahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Abu Mahdi al-Muhandis na mashahidi wengine walioandamana nao.

Siku chache zilizopita Masoud Barzani, Mkuu wa chama cha Demokrasia cha Kurdistan huko Iraq, katika mahojiano aliyoyafanya na televisheni ya MBC ya nchini Saudi Arabia, alikiri kuwa Iran kupitia Luteni Jenerali Shahidi Qassem Soleimani ilikuwa ya awali kabisa kulisaidia eneo la Kurdistan ya Iraq kuendesha vita dhidi ya kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS).

.............
340