Main Title

source : parstoday
Jumatano

22 Aprili 2020

07:13:39
1028575

Zarif: Kuuawa shahidi Qassem Soleimani hakutabadili uungaji mkono wa Iran kwa muqawama

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC, hakutabadili mwelekeo wa uungaji mkono wa Iran kwa muqawama na mapambano yake dhidi ya ugaidi katika eneo la magharibi mwa Asia

(ABNA24.com) Mohammad Javad Zarif, aliyasema hayo Jumatatu ya jana katika mazungumzo yake na Rais Bashar Al-Assad wa Syria ambapo pia ametoa shukurani kwa wawakilishi wa Syria kufika nchini Iran kwenye marasimu ya mazishi ya Qassem Soleimani.

Kadhalika waziri wa mambo ya nje wa Iran sambamba na kutoa shukuran kwa ujumbe wa pole wa Rais Bashar Al-Assad kuhusu wahanga wa virusi vya Corona nchini Iran amesema kuwa, hivi sasa nia halisi ya Marekani katika kuyawekea vikwazo vya kidhalimu mataifa kadhaa tena katika mazingira haya magumu ya kupambana na virusi vya corona, imebainika wazi kwa kila mtu.

Mohammad Javad Zarif pia amebadilisha mawazo na Rais Asad kuhusu mawasiliano ya simu ya Jumapili iliyopita na Geir Pedersen, Mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Katika Masuala ya Syria, mashauriano ambayo yanatazamiwa kufanyika hivi karibuni kati ya Iran, Uturuki na Russia kama nchi wadhamini wa mwenendo wa mazungumzo ya Astana, majadiliano ya hivi karibuni kuhusiana na matukio ya Syria, ikiwemo kamati ya kubuni katiba, matukio ya Idlib na pia mwenendo wa kisiasa wa nchi hiyo.

Kwa upande wake Rais Bashar Al-Assad wa Syria ametoa pole kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na kupoteza maisha raia wa Iran kutokana na virusi vya Corona.

Kadhalika ameashiria nafasi isiyo na mbadala ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC katika vita dhidi ya ugaidi nchini Syria, na kutoa shukurani za dhati kwa ushirikiano mzuri uliopo kati ya Iran na Syria kuhusu mapambano ya ugaidi. Mohammad Javad Zarif, aliwasili Syria jana Jumatatu akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa kisiasa wa Iran.

...........
340