Main Title

source : parstoday
Ijumaa

22 Mei 2020

10:35:55
1039330

Kiongozi Muadhamu: Mhalifu mkuu wa maafa ya Palestina ni serikali za Magharibi na siasa zao za kishetani

Ayatullah Ali Khameni, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria ukubwa wa maafa ya kughusubiwa nchi ya Palestina na kubuniwa kwa donda la saratani la uzayuni na kusisitiza kwamba mhalifu mnkuu wa maafa ya Palestina ni serikali za nchi za Magharibi na siasa zao za kishetani.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Akizungumza leo Ijumaa mchana kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds, Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran ulifungua ukurasa mpya wa mapambano kwa ajili ya ukombozi wa taifa la Palestina na kuongeza kuwa, hatua ya mwanzo ambayo ni ya kufanyika juhudi za kuwafukuza Wazayuni katika ardhi za Wapalestina na kuimarishwa harakati za kisiasa kwa lengo hilo, yote hayo yamepelekea kudhihiri kwa 'Mrengo wa Muqawama' (mapambano ya Kiislamu) katika eneo zima la Asia Magharibi na hivyo kuibua moyo wa matumaini ya kutatuliwa suala la Palestina.

Kiongozi Muuadhamu amesema, leo mrengo wa muqawama unaendelea kuimarika kila siku kinyume na mrengo wa dhulma, kufr, na uistikbari ambao unaendelea kudhoofika na kukata tamaa. Amesema jambo hilo linathibitishwa wazi na ukweli kwamba hii leo jeshi la utawala ghasibu na wa Kizayuni wa Israel ambalo wakati mmoja lilichukuliwa kuwa ni jeshi lisiloshindwa katika eneo la Asia Magharibi hii leo linapigishwa makoti na kudhalilishwa na wapiganaji wa makundi ya wananchi na Kiislamu katika nchi za Lebanon Ukanda wa Gaza na kulazimishwa kuondoka katika ulizozikalia kwa mabavu.

Habari zaidi kuhusiana na hotuba hiyo ya Kiongozi Muadhamu zitakujieni katika matangazo yetu ya usiku.

342/