Main Title

source : parstoday
Jumapili

5 Julai 2020

11:25:56
1052755

Ufuatiliaji kisheria na kisiasa wa faili la kuuawa shahidi Qassem Soleimani na wenzake

Ufuatiliaji kisheria na kisiasa wa faili la kuuawa shahidi Luteni Qassem Soleimani, Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Sepah pamoja na wenzake aliokuwa ameandamana nao huko Iraq umewekwa katika ajenda ya Baraza la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika uwanja huo kikao maalumu kilifanyika siku ya Jumamosi katika sekritarieti ya baraza hilo ambapo viongozi wa idara mbalimbali za kisheria, kisiasa, kiusalama na kijeshi walikutana na kuchukua uamuzi wa kufuatilia haraka faili hilo.

Muhsin Baharvand, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anayeshughulikia masuala ya kisheria na kimataifa alisema kuwa tayari watu waliohusika na mauaji ya Shahidi Soleimani wamekwishatambuliwa na kwamba wengine wakiwemo wanaorusha angani droni za Marekani nchini Iraq watatambuliwa hivi karibuni.

Akibainisha katika kikao hicho hatua ambazo zimechukuliwa hadi sasa katika kufuatilia faili la mauaji hayo ya kigaidi, al-Qasi Mehr, Mwendesha Mashtaka wa mjini Tehran  alisema: Watu 36 ambao walihusika moja kwa moja au kutoa amri ya kuuawa kigaidi Haj Qassem Soleimani, wawe ni viongozi wa kisiasa au kijeshi wa Marekani na serikali nyingine tayari wamekwishajulikana na tayari viongozi wa vyombo vya sheria wameshatoa alama nyekundu dhidi yao na kuitaka polisi ya kimataifa ya Intrepol isadie katika kukamatwa kwao.

Mwendesha Mashtaka wa Tehran amesema kwamba watu hao wanatuhumiwa kwa makosa ya mauaji na ugaidi, na kuwa wanaoongoza katika orodha hiyo ni Rais Donald Trump wa Marekani na kwamba atafuatiliwa kisheria hata baada ya kuondoka uongozini.

Alfajiri ya tarehe 3 Januari mwaka huu, magari yaliyokuwa yamewabeba Luteni Qassem Soleimani, Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Sepah, na ambaye alikuwa ameelekea nchini Iraq kutokana na mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo pamoja na wenzake 10 raia wa Iran na Iraq akiwemo Abu Mahdi al-Muhandis, naibu mkuu wa askari wa Hashd as-Sha'bi na msemaji wa kundi hilo la wanaharakati, yalilengwa kwa mabomu yaliyodondoshwa na droni za Marekani zilizoko nchini Iraq, hatua ya kigaidi ambayo ilipelekea kuuawa watu wote waliokuwa kwenye msafara huo wa magari.

Viongozi wa Marekani walithibitisha rasmi kwamba shambulio hilo la kigaidi lilitekelezwa kwa amri ya moja kwa moja ya rais wa nchi hiyo.

Kwa mtazamo wa sheria za kimataifa, kulengwa kwa silaha viongozi wa serikali ya nchi nyingine ni mfano wa wazi wa kuhujumiwa utawala wa nchi hiyo. Kwa msingi huo hatua hiyo ya kigaidi ya Marekani katika ardhi ya Iraq  dhidi ya makamanda hao, ni jambo linaloweza kufuatiliwa kisheria na viongozi wa Iraq.

Marekani iliwalenga moja kwa moja makamanda hao wa Iraq na Iran ambao kwa muda mrefu walikuwa wametoa pigo kubwa kwa magaidi wa Daesh wanaodhaminiwa na nchi hiyo ya Magharibi dhidi ya maslahi ya Waislamu.

Kama alivyosema Ali Shamkhani, Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na ambaye pia ni Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa katika kikao cha siku ya Jumamosi; Chuki ya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Shahid Luteni Qassem Soleimani na Shahidi Abu Mahdi al-Muhandis ilitokana na nafasi yao muhimu katika mapambano dhidi ya ugaidi na utakfiri katika eneo na ufichuaji wao wa madai ya uongo ya Marekani dhidi ugaidi.

Jambo lisilo na shaka ni kuwa Shambulio la kigaidi lililotekelezwa na Marekani Januari mwaka huu katika ardhi ya Iraq dhidi ya Luteni Shahidi Qassem Soleimani na wenzake aliokuwa ameandamana nao ni mfano wa wazi kabisa wa ugaidi unaodhaminiwa kiserikali na ambao unakiuka misingi yote ya sheria za Umoja wa Mataifa na hasa kipengee cha 2 na mada ya 4 ya sheria hizo zinazopiga marufuku kila aina ya ukiukaji dhidi ya utawala, ardhi na kujitawala kisiasa kwa mataifa ya dunia.

Kwa kuzingatia hilo ni wazi kuwa kuna udharura wa kufuatiliwa ukiukaji wa Marekani wa sheria za kimataifa katika faili hilo la mauaji ya kigaidi katika taasisi na mashirika ya kisiasa ya kimataifa. Bila shaka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kufuatilia suala hilo kwa nguvu zake zote katika taasisi husika za kimataifa.

342/