Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

10 Julai 2020

09:45:04
1054048

Faili la mauaji ya kigaidi ya Soleimani lawasilishwa mbele ya Baraza la Haki la UN

Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa amesema Marekani imeiweka dunia katika hatari kubwa ambayo haijawahi kushuhudiwa tena kutokana na hatua ya jeshi lake kumuua Luteni Jenerali Qassem Soleimani, kamanda shahidi wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC).

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Agnès Callamard alisema hayo jana Alkhamisi wakati akikabidhi ripoti yake juu ya mauaji hayo ya kigaidi kwa Baraza la Haki za Binadamu la UN na kusisitiza kuwa, wakati umefika kwa jamii ya kimataifa kuvunja kimya chake juu ya mauaji ya kiholela yanayofanywa na Washington kwa kutumia ndege zisizo na rubani 'drone.' 

Callamard ameliambia Baraza la Haki za Binadamu la UN kuwa, "mauaji hayo ya Januari 3 yameweka kumbukumbu na mfano hatari, sambamba na kuiweka dunia katika ncha ya jabali."

Amelitaja shambulizi hilo kama tukio la kwanza kuwahi kunakiliwa, ambapo dola limetumia kile lilichokitaja kama 'kujihami' kuhalalisha mauaji ya afisa wa serikali nje ya eneo liiloshuhudia mgogoro wa kivita.  

Kabla ya kukabidhi ripoti yake kwa Baraza la Haki za Binadamu la UN hapo jana, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji yanayofanywa kinyume cha sheria alisema Marekani imeshindwa kutoa ushahidi wa kutosha wa kuyapa nguvu madai yake kwamba Jenerali Soleimani alikuwa tishio kwa taifa hilo.

Afisa huyo wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa anasisitiza kuwa, mauaji hayo ya kigaidi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani yalikiuka sheria za kimataifa na Hati ya UN.

342/