Main Title

source : parstoday
Jumatatu

13 Julai 2020

09:50:47
1054784

Mrengo wa al-Fat'h Iraq: Serikali iharakishe mashtaka dhidi ya Marekani UN kwa mauaji ya Al-Muhandis

Muungano wa al-Fat'h katika Bunge la Iraq umeitaka serikali iharakishe mchakato wa kuwasilisha rasmi mashtaka Umoja wa Mataifa ya jinai iliyofanywa na Marekani ya kumuua kigaidi Abu Mahdi al-Muhandis, Naibu Mkuu wa al-Hashdu-Sha'abi.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Muungano wa al-Fat'h aidha umelitaka bunge la Iraq liunde tume maalumu itakayojumuisha kamati ya uhusiano wa nje na wizara ya sheria kwa ajili ya kufuatilia hatua za serikali na mashtaka itakayowasilisha Umoja wa Mataifa.

Muungano huo vile vile umesema, kulaaniwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kitendo cha Marekani cha kutumia ndege za ujasusi kwa ajili ya kumuua kigaidi Shahidi Qassem Soleimani ni hatua chanya na ukaongeza kuwa, una matumaini Umoja wa Mataifa utachukua misimamo ya kishujaa zaidi kukabiliana na jeuri ya Marekani ya kukiuka mamlaka ya utawala ya nchi zingine na uchukuaji mara kwa mara hatua za kiuadui katika nchi hizo.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), ambaye tarehe 3 Januari 2020 alielekea nchini Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo, aliuliwa shahidi yeye pamoja na Abu Mahdi al-Muhandis, Naibu Mkuu wa al-Hashdu-Sha'abi na watu wengine wanane waliokuwa wameandamana nao, katika shambulio la kigaidi la anga lililofanywa na jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad, Iraq.../


342/