Main Title

source : Parstoday
Jumatano

26 Agosti 2020

11:36:21
1065618

Harakati ya IMN yataka kufanyike uchunguzi kuhusu mashambulizi dhidi ya waomboleza wa Muharram, Nigeria

Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) imetoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu shambulizi lililofanywa na polisi ya nchi hiyo dhidi ya Waislamu waliokuwa katika shughuli ya kidini ya kukumbuka mauaji ya mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) katika jimbo la Kaduna.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Taarifa iliyotolewa na harakati hiyo imesema: Kwa kutilia maanani ushahidi uliopo ikiwa ni pamoja na nyaraka zilizotolewa na polisi baada ya shambulizi dhidi ya raia waliokuwa kwenye shughuli hiyo ya kidini, tunamtaka Mkaguzi Mkuu wa Polisi ya Nigeria kuanzisha uchunguzi mara moja kuhusu tukio hilo.

Alasiri ya Jumamosi iliyopita polisi wa jimbo la Kaduna nchini Nigeria walishambulia mkusanyiko wa Waislamu waliokuwa katika majlisi ya kukumbuka mauaji ya mjukuu wa Mtume Muhammad (saw), Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib (as) na kuua shahidi watu wawili. Idadi kadhaa ya Waislamu pia walijeruhiwa. 

Shughuli hiyo ya kidini iliandaliwa na Harakati ya Kiislamu ya Nigeria inayoongozwa na Sheikh Ibrahim Zakzaky. 

Polisi ya Nigeria imekuwa ikishambulia mikusanyiko na shughuli za kiibada zinazofanywa na Waislamu katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. 

Disemba mwaka 2015 jeshi la Nigeria lilivamia Huseiniya ya Baqiyatullah katika mji wa Zaria na kuua Waislamu wasiopungua 1,000 waliokuwa katika shughuli za kukumbuka mauaji ya Imam Hussein (as) wakiwemo watoto watatu wa kiume wa Sheikh Zakzaky.

Kiongozi wa Harakati ya Kislamu Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe Malama Zeenat walitiwa nguvuni katika hujuma hiyo na wangali wanashikiliwa na vyombo vya ualama vya Nigeria.    

342/