Main Title

source : Parstoday
Jumanne

22 Desemba 2020

15:21:20
1098484

Mjumbe wa Baraza la Kisiasa la Harakati ya An-Nujabaa ya Iraq amesema, ubalozi wa Marekani mjini Baghdad si kituo cha kidiplomasia bali ni kambi ya jeshi la nchi hiyo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Haidar al-Lami ameeleza kwamba, shambulio la karibuni dhidi ya ubalozi wa Marekani limefanywa kwa nia ovu; na lengo lake ni kuuelekezea kidole cha tuhuma muqawama na kuunufaisha mpango wa kuendelea kuwepo kijeshi Marekani nchini Iraq.

Jumapili usiku duru za habari ziliripoti kuwa, maroketi kadhaa yamefyatuliwa kuulenga ubalozi wa Marekani mjini Baghdad.

Wakati huohuo, Mkuu wa Baraza la Kisiasa la Harakati ya An-Nujabaa Ali al-Asadi ameikosoa serikali ya Iraq kwa kutochukua hatua yoyote ya maana kuhusiana na mashtaka yaliyowasilishwa dhidi ya kitendo cha kigaidi cha Marekani cha kumuua shahidi Kamanda Qassem Suleimani, mkuu wa zamani wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na Abu Mahdi al-Muhandis, aliyekuwa Naibu Mkuu wa vikosi vya Al-Hashdu-Sha'abi na akasema,  kitendo hicho cha kijinai cha Marekani ni kielelezo na mfano hai na wazi wa ugaidi na ukiukaji mamlaka ya kujitawala ya Iraq.

Luteni Jenerali Qassem Suleimani, ambaye mnamo tarehe 3 Januari mwaka huu wa 2020 alikuwa ameelekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo, aliuliwa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al-Muhandis na watu wengine wanane, katika shambulio la anga lililofanywa na jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad.

Jinai hiyo ya kigaidi ya Marekani ilipelekea siku mbili baadaye Bunge la Iraq kupitisha mswada wa kutataka majeshi yote ya kigeni yakiwemo ya Marekani yaondoke katika ardhi ya nchi hiyo.../


342/