Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

26 Desemba 2020

13:06:57
1099728

Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Shahidi Luteni Qassem Soleimani alikuwa mbeba bendera ya mapambano yaliyopelekea kusambaratishwa kundi la kigaidi la ISIS au Daesh katika eneo la Asia Magharibi na hata dunia nzima.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Brigedia Jenerali Kioumars Heidari Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu la Iran amesema Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu alikuwa shakhsia wa kipekee katika historia ya mapabano dhidi ya ugaidi. Ameongeza kuwa Shahidi Soleimani alifanikiwa kuwaangamiza maadui katika uhai wake na hata baad aya kuuawa shahidi.

Brigedia Jenerali Heidari amesema ingawa wengine walikuwa pia katika vita dhidi ya ISIS, lakini Luteni Jenerali Soleimani alikuwa na nafasi muhimu na ya kipekee katika kuangamiza kundi hilo katika eneo na duniani.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) alielekea Iraq kufuatia mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo aliuawa shahidi tarehe 3 Januari mwaka huu katika shambulio la anga la wanajeshi vamizi na magaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad Iraq akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq (Hashdu Shaabi) na wenzao wanane. Kamanda Soleimani alikuwa safarini nchini Iraq kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo.

342/