Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

28 Desemba 2020

07:42:20
1100350

Wairaqi waandamana kulaani Marekani kwa kuwaua makamanda wa vita dhidi ya ugaidi

Watu wa Iraq wameandamana katika mji mkuu, Baghdad, kulaan kitendo cha kigaidi cha Marekani cha kuwaua makamanda wakuu wa vita dhidi ya ugaidi, Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na mwanamapmabano mwenza wa Iraq Abu Mahdi al Muhandis.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Maandamano hayo ambayo yamefanyika katika Medani ya Tahrir mjini Baghdad ikiwa inakaribia mwaka moja tokea Marekani itekeleza hujuma ya kigaidi iliyopelekea makamanda hao kuuawa.

Katika maandamano hayo ambayo aghalabu ya washiriki wake walikuwa ni wanamapambano wa Jeshi la Kujitolea la Wananchi maarufu kama Hashd al Sha’abi waandamnaji wamelaani vikali ugaidi wa Marekani .

Miji mingi ya Iraq imepambwa kwa picha za mashahidi Soleimani na Al-Muhandis katika siku hizi za kukaribia maadhimisha ya kuuawa shahidi makamanda hao  wawili wa vita dhidi ya ugaidi.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) alielekea Iraq kufuatia mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo aliuawa shahidi tarehe 3 Januari mwaka huu katika shambulio la anga la wanajeshi vamizi na magaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad Iraq akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq (Hashdu Shaabi) na wenzao wanane. Kamanda Soleimani alikuwa safarini nchini Iraq kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo.

342/