Main Title

source : Parstoday
Jumanne

29 Desemba 2020

17:29:11
1100920

Iran inawafuatilia watuhumiwa 48 katika faili la mauaji ya shahid Qassem Suleimani

Katibu wa Tume ya Haki za Binadamu ya Idara ya Mahakama ya Iran amesema, watu 48 wametambuliwa kuhusika na mauaji ya kigaidi ya Luteni Jenerali Qassem Suleimani na hatua zinazohitajika zimesha chukuliwa kwa ajili ya kuwafuatilia watu hao.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ali Baqeri Kani ameeleza kwamba, nchi zote ambazo zimehusika na kushirikishwa kwa namna fulani katika jinai ya mauaji ya Kamanda Qassem Suleimani zimeombwa kuipatia Idara ya Mahakama ya Iran taarifa na nyaraka zilizonazo.

Baqeri Kani amebainisha kuwa, kwa mujibu wa ripoti na taarifa zilizopo, kituo cha jeshi la anga la Marekani cha Ramstein kilichoko nchini Ujerumani kilihusika katika mabadilishano ya taarifa za kiintelijensia baina ya ndege zisizo na rubani za Marekani ambazo zilishiriki katika jinai ya mauaji ya kigaidi ya Luteni Jenerali Qassem Suleimani.

Luteni Jenerali Qassem Suleimani, Kamanda wa zamani wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, aliuawa shahidi alfajiri ya kuamkia Ijumaa ya tarehe 3 Januari 2020 pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, aliyekuwa Naibu Mkuu wa Al-Hashdu-Sha'abi pamoja na wenzao wengine wanane katika shambulio la anga lililofanywa na jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad nchini Iraq.../

342/