Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

31 Desemba 2020

12:44:19
1101610

Hatua ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ya kuweka bango kubwa la picha ya Shahidi Qassem Soleimani, katikati ya mji wa Ghaza kimeutia hofu na woga mkubwa utawala wa Kizayuni.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Televisheni ya al Alam imeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, msemaji wa waziri mkuu wa msemaji wa jeshi la kigaidi la utawala wa Kizayuni wa Israel wametumia kurasa zao za mtandao wa kijamii wa Twitter kuonesha chuki na hasira zilizoambatana na woga kutokana na hatua hiyo ya HAMAS ya kubandika bango la picha ya shahid Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds, cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH.

Ripoti ya televisheni hiyo imeongeza kuwa, Wazayuni wametekwa na propaganda za televisheni za vibaraka wao wa Saudia, Imarati, Bahrain n.k, ambao wako mstari wa mbele katika kutangaza uhusiano wa kawaida na Israel na kusaliti malengo matakatifu ya Palestina. Televisheni za vibaraka hao zinatangaza kwamba Luteni Jenerali Qassem Soleimani alikuwa kiongozi wa wanamgambo tu, lakini Bin Salman na Bin Zayed eti ndio viongozi wa Waarabu.

Hata hivyo baada ya wakazi wa Ukanda wa Ghaza, kuweka bango kubwa la picha ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani katika barabara kuu ya al Rashid, katikati ya Ghaza ikipambwa na matamshi ya Ismail Hania, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya HAMAS, hatua hiyo imezidisha hofu katika nyoyo za Wazayuni na vibaraka wao na kuwalazimisha waoneshe wazi chuki na woga wao. 

Sehemu nyingine ya ripoti hiyo imesema, hatua hiyo ya HAMAS imeonesha kwamba uhakika wa mambo ni kinyume na walivyokuwa wakidanganywa Wazayuni na vibaraka wao na kwamba shahid Qassem Soleimani ni shahid wa Quds, ni mkombozi wa Kibla cha Kwanza cha Waislamu.

342/