Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

31 Desemba 2020

12:48:59
1101615

Rais Rouhani: Shahidi Qassim Suleimani amewazawaidia izza Waislamu na kuwadhalilisha maadui

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, shahdi Luteni Jenerali Qassim Suleimani amelizawadia izza wakazi wote wa eneo la Asia Magharibi na Waislamu wa eneo hili na amewadhalilisha maadui katika matukio mengi.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rais Rouhani amesema hayo leo katika hafla ya uzinduzi wa miradi ya kitaifa katika Wizara ya Nishati ya Iran ambapo sambamba na kuashiria kuwadia hauli na mwaka mmoja wa kumbukumbu ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassim Suleimani na kubainisha kwamba, hapana shaka kuwa maadui wamepata hasara kwa mauaji haya ya kutisha.

Dakta Rouhani ameeleza kwamba, hapana shaka yoyote kuwa, vijana, wananchi wa Iran na wa eneo la Asia Magharibi kwa ujumla wataendelea kuwa na matumaini zaidi na kusimama kidete zaidi katika njia ya mapambano na kupigania mamlaka ya kujitawala.

Rais wa Iran amesea pia kuwa, madhali Marekani ingalipo katika eneo la Asia Magharibi, basi eneo hili haliwezi kushuhudia amani na utulivu na muda si mrefu wananchi wa eneo hili watawafukuza wavamizi watenda jinai katika eneo hili.

Luteni Jenerali Qassem Suleimani, Kamanda wa zamani wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH), aliuawa shahidi alfajiri ya kuamkia Ijumaa ya tarehe 3 Januari 2020 pamoja na Abu Mahdi al-Muhandis, aliyekuwa Naibu Mkuu wa Al-Hashdu-Sha'abi pamoja na wenzao wengine wanane katika shambulio la anga lililofanywa na jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad nchini Iraq.

342/