Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

2 Januari 2021

08:32:28
1102147

Majina ya watuhumiwa wa mauaji ya shahid Soleimani kutangazwa karibu hivi

Kiongozi mmoja wa harakati ya kujitolea ya wananchi wa Iraq maarufu kwa jina la al Hashd al Shaabi amesema kuwa, siku chache zijazo idara ya mahakama ya Iraq itatangaza majina ya watuhumiwa wa mauaji ya makamanda wa muqawama akiwemo shahid Luteni Jenerali Qassem Soleimani.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mtandao wa habari Saberin News umemnukuu Mohannad al Aqabi, mkurugenzi wa vyombo vya habari wa harakati ya al Hashd al Shaabi akisema hayo usiku wa kuamkia leo Jumamosi na kuongeza kuwa, kuna watuhumiwa 40 katika kesi ya mauaji ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH baadhi yao ni Wairaq na wengine ni Wamarekani.

al Aqabi amesisitiza kuwa, licha ya kwamba idadi ya mahakama ya Iraq iko chini ya mashinikizo ya ndani na nje, lakini imefanya kazi kubwa ya kuwatambua watuhumiwa na siku chache zijazo majina ya watuhumiwa hayo yatatangazwa hadharani.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Mkuu wa Kikosi cha Quds, cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, Abu Mahdi al Muhandis, Naibu wa Mkuu wa Harakati ya al Hashd al Shaabi na wanamapambano wenzao wanane, waliuliwa kigaidi na kidhulma na wanajeshi magaidi wa Marekani, tarehe 3 Januari 2020 katika shambulio la anga lililofanywa na magaidi hao karibu na uwanja wa ndege wa Iraq, akiwa mgeni rasmi wa serikali ya nchi hiyo.

342/