Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

2 Januari 2021

08:34:06
1102149

Jenerali Baqeri: Kisasi kikali kwa wauaji wa Shahidi Suleimani muda wake hauishi

Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kisasi cha mauaji ya kigaidi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC kitakuwa kikali na wala hakina muda wa kumalizika.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Brigedia Jenerali Mohammad Baqeri alisema hayo jana Alkhamisi na kueleza bayana kuwa, kuondoka askari vamizi wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi ni jambo lisiloepukika.

Brigedia Jenerali Baqeri amesema hayo katika ujumbe wake kwa mnasaba wa kukaribia kumbukumbu ya mwaka mmoja tokea auawe Shahidi Jenerali Suleimani na kusisitiza kuwa, Iran na mataifa ya Kiislamu na yenye kupenda uhuru duniani yamejitolea kwa dhati kulipiza kisasi kwa waliotoa amri na kutekeleza jinai hiyo ya kigaidi.

Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Jenerali Suleimani ni nembo ya kimataifa ya muqawama, na waungaji mkono wote wa muqawama na mapambano wako tayari kulipiza kisasi cha damu ya Shahidi huyo.

Brigedia Jenerali Baqeri amesisitiza kuwa: Januari 3 ni kumbukumbu ya tukio chungu katika historia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambapo shujaa aliyeisambaratisha Daesh (ISIS)- kundi hatari zaidi la kigaidi na kitafiri lililozalishwa na kulelewa na Marekani na vibaraka wake; kwa ajili ya usalama wa mataifa hususan Umma wa Kiislamu- aliuawa kiwoga na adui mkubwa na nambari moja wa ulimwengu wa Kiislamu, yani dola la kiistikbari na kigaidi la Marekani.

Siku chache baada ya majeshi ya kigaidi ya Marekani kumuua shahidi Jenerali Suleimani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad tarehe 3 Januari mwaka uliomalizika, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu lilishambulia kwa makumi ya makombora kambi za jeshi la Marekani katika mkoa wa Al-Anbar na Erbil nchini Iraq.

342/