Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

2 Januari 2021

08:37:52
1102152

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema harakati za hivi karibuni za kijeshi za Marekani katika eneo zinatokana na makosa ambayo nchi hiyo imeyatenda mwaka uliopita kwa kuwaua kigaidi Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi Al Muhandis na kuongeza kuwa: "Iran iko tayari kutoa jibu kwa chokochoko zozote zile za adui katika eneo."

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Meja Jenerali Hussein Salami Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyasema hayo Ijumaa mjini Tehran pembizoni mwa hafla ya mwaka wa kwanza wa kukumbuka mauaji ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Abu Mahdi al Muhandis na wenzao kadhaa. Ameongeza kuwa, jinai ya Marekani katika kuwaua makamanda hao wa muqawama iliumiza nyoyo za vijana katika ulimwengu wa Kiislamu na kuongeza kuwa machungu hayo mengi yatabakia daima kuwa kama jinamizi litakaloisakama Marekani.

Meja Jenerali Salami ameongeza kuwa katika kujiondoa katika jinamizi hilo hatari, Wamarekani sasa wameanzisha msururu wa chokochoko.

Kamanda Mkuu wa IRGC amesisitiza kuhusu kuendelezwa njia ya mashahidi ya muqawama na mapambano na kusema: "Vijana wa ulimwengu wa Kiislamu leo, zaidi ya wakati wowote ule, wana irada imara imara ya kuwatimua Wamarekani katika eneo na kuwashinda kikamilifu Wazayuni.

Brigedia Jenerali Salami ameashiria kuendelea mchakato wa ulipizaji kisasi mgumu ambao umeanza katika eneo na kusema: "Ulipizaji kisasi huo si wa mara moja bali ni mchakato; yaani walioshiriki katika jinai hiyo hawataweza kutulia." Aidha amesema mazingira ndiyo yatakayobaini zama , eneo na kiwango cha ulipizaji kisasi.

Kamanda Mkuu wa IRGC ameongeza kuwa kuanza kusambaratika utawala wa Kizayuni wa Israel na kuangamiza satwa ya kibeberu ya Marekani katika eneo ili Waislamu waweze kujiamulia hatima yao ni kati ya mchakato huo wa ulipizaji kisasi mauaji ya makamanda wa muqawama.

342/