Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

2 Januari 2021

08:39:58
1102153

Leo Jumamosi, tarehe pili Januari 2021 inayosadifiana na tarehe 13 Dei 1399 mwaka wa Kiirani wa Hijria Shamsia, inasadifiana na mwaka mmoja tangu alipouawa shahidi na kidhulma, Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi SEPAH.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha SEPAH, Abu Mahdi al Muhandis, Naibu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Iraq maarufu kwa jina la al Hashd al Shaabi pamoja na wenzao wanane, waliuliwa kikatili na jeshi la kigaidi la Marekani, tarehe 3 Januari 2020, kwenye shambulio la anga lililofanywa na magaidi hao wa Marekani, karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad, mji mkuu wa Iraq.

Kamanda Soleimani ambaye amepewa lakabu ya bwana wa mashahidi wa muqawama, katika umri wake wote uliojaa baraka na akiwa kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH alikuwa mstari wa mbele kuyasaidia na kuyaunga mkokno mataifa yanayodhulumiwa ya Waislamu bila ya kujali ni mataifa ya watu gani. Muhimu kwake muda wote ilikuwa ni kupigania Uislamu na mafundisho ya Qur'ani Tukufu.

Akiwa MKuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, Luteni Jenerali Qassem Soleimani alifanikiwa kuliangamiza genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) katika nchi mbili za Kiarabu za Iraq na Syria na alifanikiwa kuwapa zawadi ya utulivu na usalama wananchi wa nchi hizo kupitia kuasisi kwake harakati za kujitolea za wananchi.

342/