Main Title

source : Parstoday
Jumapili

3 Januari 2021

08:24:43
1102549

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo amezindua stempu ya kumbukumbu ya Shahidi Qassem Soleimani.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa taarifa,  sambamba na kuwadia mwaka mmoja tokea auawe shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Rais  Hassan Rouhani  wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo Jumamosi amezindua stempu maalumu iliyopewa jina la 'Kamanda wa Nyoyo".

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Mkuu wa Kikosi cha Quds, cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, Abu Mahdi al Muhandis, Naibu wa Mkuu wa Harakati ya al Hashd al Shaabi na wanamapambano wenzao wanane, waliuliwa kigaidi na kidhulma na wanajeshi magaidi wa Marekani, tarehe 3 Januari 2020 katika shambulio la anga lililofanywa na magaidi hao karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad nchini Iraq, akiwa mgeni rasmi wa serikali ya nchi hiyo.

Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani alikuwa na nafasi kubwa katika mapambano na maadui pamoja na magaidi na pia katika kuangamiza kundi la kigaidi la Daesh au ISIS. Pia alikuwa nguzo muhimu katika harakati za kupigania ukombozi wa Palestina. Halikadhalika alikuwa na nafasi muhimu katika kusambaratisha njama ya Marekani na Wazayuni ya kuligawa vipande vipande eneo la Asia Magharibi.

342/