Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

4 Januari 2021

09:34:08
1102939

Kumbukumbu za mwaka mmoja wa tangu kuuawa kigaidi, shahid Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Iraq maarufu kwa jina la al Hashd al Shaabi, zimefanyika katika mji wa Kano nchini Nigeria.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Twitter wa Sheikh Ibrahim Zakzaky, mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria umeandika kwamba kumbukumbu hizo zimefanyika mjini Kano na umeweka picha za kumbukumbu hizo ambazo zimehudhuriwa na idadi kubwa ya Waislamu wa Nigeria.

Kamanda Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al Muhandis pamoja na wanamapambano wenzao wanane, waliuliwa kidhulma na wanajeshi magaidi wa Marekani, tarehe 3 Januari 2020 katika shambulio la anga lililofanywa kwa amri ya rais wa Marekani, Donald Trump, karibu na Uwanja wa Ndege wa Baghdad, mji mkuu wa Iraq.

Kamanda Soleimani alikwenda nchini Iraq kwa mwaliko wa serikali ya nchi hiyo, lakini Wamarekani hawakuheshimu hata protokali za kidiplomasia na walimuua uraiani shujaa ya huyo wa vita dhidi ya ugaidi. Nchi, taasisi na makundi mengi duniani yamelaani jinai hiyo ya kigaidi ya Marekani.

Hadi al Amiri, Katibu Mkuu wa taasisi ya Badr ya Iraq, siku ya Ijumaa alisema kuwa, shahid Soleimani daima alikuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya magenge ya kigaidi na ameuawa shahidi katika njia ya kupigania usalama wa Iraq.

342/