Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

4 Januari 2021

09:37:05
1102941

Mkuu wa Al-Hashdu-Sha'abi: Tutaendelea kuienzi damu toharifu ya makamanda wa ushindi

Mkuu wa Al-Hashdu-Sha'abi ya Iraq amesema, hatua ya mwanzo kabisa ya kulipiza kisasi cha mashahidi Qassem Suleimani na Abu Mahdi al-Muhandis ni kula kiapo tena cha utiifu kwao na kuendeleza njia yao.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Falih al-Fayyaz ameyasema hayo alifajiri ya kuamkia leo katika hotuba aliyotoa mahali walipouliwa kigaidi mashahidi hao wa muqawama na akaeleza kwamba Al-Hashdu-Sha'abi ni umma mmoja; na umma huo utaendelea kuzienzi damu toharifu zilizomwagwa na kulinda malengo na thamani tukufu zilizotiliwa mkazo na makamanda wa ushindi.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Iraq Abu Hussein al-Hamidawi, ambaye naye pia alihutubia hauli na maadhimisho hayo ya mwaka wa kwanza wa kumbukumbu ya kuuawa shahidi makamanda wa muqawama, amesisitiza kuhusu udharura na ulazima wa kudumisha silaha ya muqawama kwa ajili ya kulinda ya ardhi ya Iraq na akabainisha kwamba, "kwa msaada wa Mwenyezi Mungu tutakuwa na Suleimani wengine elfu moja na Abu Mahdi wengine elfu moja pia."

Mapema leo asubuhi, maelfu kwa maelfu ya wananchi wa Iraq walielekea kwenye uwanja wa mzunguko wa At-Tahrir mjini Baghdad kushiriki katika maandamano makubwa yaliyopewa anuani ya "Kufa Shahidi na Kujitawala" kwa mnasaba wa kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa kuuawa shahidi Kamanda Suleimani na Al Muhandis.

Alfajiri ya kuamkia siku kama ya leo mnamo Januari 3,2020 Luteni Jenerali Qassem Suleimani, Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, Abu Mahdi al Muhandis, Naibu wa Mkuu wa Harakati ya al Hashdu-Sha'abi na wanamapambano wenzao wanane, waliuliwa kigaidi na kidhulma na wanajeshi magaidi wa Marekani, katika shambulio la anga lililofanywa na magaidi hao karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad nchini Iraq.../

342/