Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

4 Januari 2021

09:42:55
1102945

Hijazi: Wanaodhani Israel itawapa amani, wajiulize je Wazayuni hata wameweza kudhamini usalama wao?

Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema kuwa, kuwepo Wazayuni katika eneo hili na hatua ya baadhi ya nchi za Ghuba ya Uajemi za kutangaza uhusiano wa kawaida na Israel ndiko kunakohatarisha usalama na utulivu wa eneo hili.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Brigedia Jenerali Mohammad Hijazi amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na televisheni ya al Mayadeen ya Lebanon na kuongeza kuwa, huenda baadhi ya watu huko Imarati na Bahrain wakadhani kwamba kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni kutawaletea amani na usalama, lakini watu hao inabidi wajiulize, huo utawala wenyewe wa Kizayuni ni kiasi gani umeweza kujidhaminia usalama wake wenyewe?

Vile vile amesema, kuna uwezekano uwepo wa Wazayuni katika eneo hili ukawa ni tishio kwa usalama wa kitaifa wa Iran na kusisitiza kuwa, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH kamwe halitokubali kuona nchi zinazopakana na Ghuba ya Uajemi zinakuwa chanzo cha vitisho kwa usalama wa kitaifa wa Iran.

Amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina msimamo usiotetereka kuhusu kuwahami na kuwaunga mkono wananchi wa Palestina akisisitiza kuwa, sasa hivi utawala wa Kizayuni hauthubutu kirahisi kuanzisha mashambulizi dhidi ya Palestina kwani unajua kwamba lazima utajibiwa na kupata hasara kubwa.

Vile vile amesema, kuwalinda wanyonge na wanaodhulumiwa ni sehemu ya malengo matukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akifafanua zaidi kwa kusema, vitendo vya adui katika eneo la Asia Magharibi kama vile kuzivamia na kuzikalia kwa mabavu nchi za Iraq na Afghanistan, kuanzisha na kuliunga mkono genge la kigaidi la Daesh (ISIS) na magenge mengine ya kigaidi, kuunga mkono jinai za Wazayunidi dhidi ya Wapalestina n,k, ni miongoni mwa mambo yaliyochangia kustawishwa na kupata nguvu Kikosi cha Quds, cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH.

342/