Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

1 Februari 2021

12:58:50
1111297

Jeshi la Myanmar latwaa madaraka ya nchi; rais na viongozi wengine watiwa mbaroni

Jeshi la Myanmar limethibitisha kulidhibiti madaraka ya nchi baada ya kumkamata Rais wa nchi na viongozi wengine akiwemo Aung San Suu Kyi mapema hii leo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Taarifa zinasema, kiongozi wa chama tawala mwenye ushawishi nchini Myanmar Aung San Suu Kyi amekamatwa na jeshi, baaada ya wanajeshi kutwaa madaraka, kufuatia siku kadhaa za mivutano nchini humo ambayo ilizua hofu ya kutokea mapinduzi.

Aidha Rais Win Myint wa Myanmar na viongozi kadhaa wa ngazi za juu wa chawa tawala pia wamekamatwa mapema leo.

Msemaji wa chama tawala cha National League for Democracy (NLD) amesema kuwa, kiongozi wa chama hicho Aung San Suu Kyi, ambaye chama chake cha kipo madarakani amekamatwa. 

Tangu wiki iliyopita jeshi la Myanmar limekuwa likitishia kufanya mapinduzi kwa madai kwamba kulifanyika udanganyifu katika uchaguzi mwezi Novemba ambao matokeo yake yanaonyesha kuwa, chama cha Suu Kyi cha NLD kiibuka na ushindi.

Wanajeshi wanaonekana mitaani katika mitaa ya mji mkuu wa Naypyitaw pamoja na mji wa Yangon. Huduma za simu na mtandao zilizimwa katika miji mikubwa wakati televisheni ya taifa inasema kwamba kulikuwa na hitilafu za kiufundi.

Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali hatua hiyo ya jeshi la Myanmar na kuwataka wanajeshi kuwaachilia huru viongozi hao.

Uchaguzi wa Bunge wa Myanmar ulifanyika katika hali ambayo, chama tawala cha Aung San Suu Kyi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kimefanyika ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na mauaji dhidi ya jamii ya walio wachache ya Waislamu wa Rohingya katika mkoa wa Rakhine.


342/