Main Title

source : Parstoday
Jumapili

7 Februari 2021

12:31:09
1113074

Kiongozi Muadhamu: Sharti la Iran la kurejea katika ahadi zake za JCPOA ni Marekani kuondoa vikwazo kivitendo

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, Iran itarejea katika ahadi zake za makubaliano ya nyuklia ya JCPOA pale Marekani itakapoliondolea taifa hili vikwazo vyake vyote tena kivitendo na sio kwa maneno matupu au katika makaratasi tu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi amesema hayo asubuhi ya leo alipokutana na makamanda na watumishi wa kikosi cha anga cha jeshi la Iran na kueleza kwamba, kiapo cha utiifu na cha kihistoria cha jeshi la anga kwa Imam Ruhullah Khomeini (MA) lilikuwa moja ya matukio muhimu na ya msingi ya kupata ushindi Mapinduzi ya Kiislamu na ilikuwa ishara ya wazi ya makosa ya kimahesabu ya Wamarekani.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, sharti la kuendelea harakati yenye kasi ya mapinduzi ni mahudhurio ya wananchi katika medani, kufanya kazi kwa hima na bidii kubwa, kuweko na umoja wa kalima hususan baina ya maafisa na viongozi wa serikali, kuwa na imani na ahadi ya Mwenyezi Mungu na kuongeza katika vitendo mambo ambayo ni sababu ya kupatikana nguvu ya kitaifa.

Ayatullah Khamenei amesema pia kuwa, matukio ya fedheha yaliyoshuhudiwa hivi karibuni nchini Marekani na kuporomoka Donald Trump ni kudhoofika hatua kwa hatua hadhi, nguvu na mfumo wa kijamii na kisiasa wa Marekani.

Kiongozi Muadhamu ameashiria matamshi ya viongozi wa Ulaya na Marekani kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na vikwazo na kusisitiza kwamba,  viongozi wa Marekani na madola ya Ulaya hawana haki ya kuweka sharti lolote lile, kwani wao ndio waliokiuka makubaliano ya nyuklia, bali Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo yenyewe imeheshimu na kufungamana kikamilifu na makubaliano hayo ndio inayopaswa kuweka sharti.

342/